Gazeti The Citizen Tanzania lafungiwa kwa siku saba


The Citizen Tanzania lafungiwa kwa siku saba

Haki miliki ya picha
Millard Ayo

Image caption

The Citizen Tanzania lafungiwa kwa siku saba

Maoni mbalimbali yametolewa kutokana na hatua ya kusimamishwa kwa leseni ya uchapishaji na usambazaji wa gazeti la The Citizen kwa siku saba.

Serikali ya Tanzania imelifungia gazeti la hilo kwa madai ya kuchapisha taarifa ya upotoshaji kuhusu maoni ya watalaam waliozungumzia kuporomoka kwa shilingi.

Kufuatia kufungiwa huko kwa gazeti hilo la kila siku, kumeibua maoni tofauti miongoni mwa wananchi, wachambuzi na wadau mbalimbali wa habari.

Mamlaka zimeshutumu gazeti hili la kila siku kukiuka maadili katika uchambuzi wake wa makala mbalimbali.Lakini makundi ya upinzani na asasi za kiraia miezi ya hivi karibuni walikosoa utawala wa Rais Magufuli kwa kukandamiza uhuru wa habari nchini Tanzania, madai ambayo yalikanushwa.

Msajili wa magazeti nchini Tanzania, Patrick Kipangula amethibitisha hilo kutokana na taarifa kuhusu kuporomoka kwa shilingi iliyochapishwa juma lililopita.Mhariri wa gazeti hilo amesema wameshtushwa na uamuzi wa serikali lakini hakuwa tayari kueleza zaidi.

Magufuli ayaonya magazeti Tanzania

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita karibu magazeti 7 , likiwemo gazeti la Mseto, Mwanahalisi, Mawio, Tanzania Daima na Raia Mwema, na sasa the citizen yamefungiwa kwa nyakati tofauti kwa makosa mbalimbali.

Wauza magazeti wameguswa na hatua hii ya serikali baadhi wanaona kuwa vipato vyao viko hatarini.” Hata kama Napata shilingi 1,500 mimi inanisaidia, kwa sababu mimi kazi yangu ni kuuza magazeti,

unavyofungia gazeti moja, mawili ama matatu, unakiathiri kipato changu na maisha yangu.” alieleza Ramadhan Ramdhan.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *