Ghadhabu baada mahakama kupunguza hukumu ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto India


File photo of an Indian boy

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Uchunguzi wa serikali ya India ulionyesha kwamba wavulana walikuwa katika hatari sawa ya kudhulumiwa

Siku mojo baada ya Mahakama ya juu zaidi nchini India kupitisha hukumu ambayo ilimuondolea hatia mtu aliyemnyanyasa kingono mtoto wa kike wa miaka kwa sababu “hakukuwa na mgusano wa ngozi kwa ngozi” na mwathiriwa, hukumu nyingine iliyopunguza kifungo cha jela kwa mwanamume aliyepatikana na hatia ya kumdhalilisha kingono mvulana wa miaka 10 imesababisha hasira.

Amri hiyo, ambayo ilitangulia uamuzi wa kihistoria wa Mahakama ya Juu kwa siku moja lakini sasa imeripotiwa, ilitangazwa na mahakama kuu ya Allahabad katika jimbo la kaskazini la Uttar Pradesh.

Uhalifu huo ambao ulifanyika mwaka wa 2016 wakati mwanamume huyo alipotembelea nyumba ya mtoto huyo na kumpeleka katika hekalu la eneo hilo ambako alimdhalilisha kingono.

Alikuwa amempatia mtoto huyo rupi 20 sawa na ( senti 27) ili kumnyamazisha asizungumzie unyanyasaji huona kumtishia endapo atatoa taarifa ya kile kilichotokea.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *