Hasara yaongezeka kwa kampuni ya ndege ya Kenya Airways


Ndege ya kampuni ya Kenya Airways

Haki miliki ya picha
KQ

Image caption

KQ inasema kuwa hasara imetokana na ongezeko kubwa bei ya mafuta, mishahara ya juu, na viwango vya juu vya gharama za usafiri wa ndege

Shirika la taifa la safari za ndege nchini Kenya Kenya Airways(KQ) limetangaza kupata hasara ya kifedha mwaka uliopita kwa takriban $75m.

Hasara hiyo ambayo ni sawa na shilingi za Kenya 7.59 ilirekodiwa katika kipindi cha miezi 12 hadi mwishoni mwa mwaka 2018.

Hata hivyo kiwango hiki cha hasara ni kidogo kuliko hasara ya mwaka jana ambayo ilikuwa ni Shilingi bilioni 9.44 katika kipindi cha mwaka 2017.

Taarifa hii imechapishwa katika ukurasa wa jarida maarufu la maswala ya uchumi na fedha:

Kampuni hiyo inasema kwa hasara imetokana na ongezeko kubwa bei ya mafuta, misjhahara ya juu, na viwango vya juu vya gharama za usafiri wa ndege vilivyowekwa na mmiliki.

Hata hivyo kulikuwa na ongezeko la mapato ya kiasi cha Shilingi bilioni 114.45 ikilinganishwa na mwaka jana ambapo yalikuwa ni Shilingi bilion 106.2. Hata hivyo mapato hayo ni chini ya mapato yao ya Shilingi 116 bilioni waliyopatikana mwaka 2016.

Image caption

Migomo ya wafanyakazi wa Shirika la ndege la Kenya Airways imeelezwa kuchangia hasara ya kampuni hiyo

Shirika hilo la ndege la kimataifa limekuwa likitumia suala la hasara linayoipata kujaribu kuchukua utawala wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, lakini Wakenya wengi wamekuwa wakielezea kutokubaliana na hoja hiyo.

Ni zipi sababu za harasa inayoipata Kenya Arways?

Kulingana na tume ripoti ya tume ya seneti iliyochukua jukumu la kuelewa mzozo wa hasara katika Kenya Airways mwaka 2015, iliyoongozwa na Seneta Anyang’ Nyong’o cha sababu tano zilibainishwa, lakini wachanganuzi wa masuala ya uchumi wanasema hakuna aliyejali kuzitafutia suluhu.

Sababu tano zilizotajwa kusababisha hasara katika KQ:

  • Maamuzi mabaya ya uwekezaji katika ununuzi na uuzaji wa ndege, makubaliano ya ununuzi wa mafuta yanayosababishia hasara kampuni na hivyo kuisababishia kampuni kuwa na madeni makubwa.
  • Uuzaji wa tiketi za bei ya juu zisizo na ushindani kwenye soko jambo linalosababisha kuwapoteza wateja na mapato.
  • Mipango mibovu ya safari na ushirikiano inayoweza kusababisha hasara kubwa ya mapato hususan kutokana na kutoongezwa kwa safari katika nchi za Afrika.
  • Matatizo ya sera ya wafanyakazi inayozosababisha mizozo ya wafanyakazi: Kwa picha mgomo wa wafanyikazi JKIA ulivyokua
  • Kufutwa mara kwa mara kwa safari na hivyo uhusiano mbaya na wasafiri, ambao mara nyingi wameacha kusafiri na ndege za kampuni.

Kenya Airways yaanza safari za moja kwa moja hadi Marekani

Marubani wasitisha mgomo wao Kenya

Baadhi ya Wakenya wamekuwa wakielezea hisia zao juu ya hasara inayoendela kulikumba shirika la ndege la taifa lao kenya Airways. Mfano picha hii ya kibonzo iliyotumwa kwenye mtandao wa kijamii inaelezea kwa kifupi hisia za baadhi ya wakenya juu ya tangazo la hasara kwa KQA :

Unaweza pia kutizama:

Huwezi kusikiliza tena

Kenya Airways yafuta safari za ndegeSource link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *