Hisia saba ambazo hazipo tena au zilizobadilika


Hisia - zinatofautina na zinabadilika kutoka kwa mtu moja hadi mwingine

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Hisia – zinatofautina na zinabadilika kutoka kwa mtu moja hadi mwingine

Mara nyingi watu hufikiria hisia za binadamu ni moja kote duniani na kwamba zinafanana.

Lakini ukweli ni kwamba hisia zinatofautina na zinabadilika kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Pia imebainika kuwa hisia mpya zinagunduliwa kadiri muda unavyosonga, kwa mfano hisia inayompata mtu akiwa na hofu huenda amekosa au akakosa kuhudhuria shughuli aliyokuwa akiikamia.

Hisia hiyo imevumbuliwa kutokana na ujio wa mitandao ya kijamii – Hii ni hisia ambayo mtu anapata akiona picha zinazowekwa mitandaoni na watu waliyohudhuria hafla ambayo yeye anatazamia kuhudhuria.

Hofu hiyo inajulikana kama FOMO kwa kimombo ”Fear Of Missing Out’ kwa wafuatilialiji wa mitandao wa kijamii.

BBC imezungumza na Dr Sarah Chaney, mtaalamu wa Kituo cha Historia ya Hisia, kubaini jinsi hisia za zamani zinavyotusaidia kuelewa jinsi tunavyohisi leo.

Hizi hapa baadhi ya hisia hizo.

1.Msongo wa mawazo

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Acedia ni hisia iliyohusishwana viongozi wa kidini wanaojipata katika

Hii ni hisia ya ambayo pia huwapata mapadriwa wa umri wa makamo ambao wanaishi chini y a kiapo cha kidini.

Mara nyingi hutokana na hali ya kutetereka kiimani. Mwathiriwa hujihisi kana kwmba amepoteza matumaini wakati azma yake ni ni kuishi maisha matakatifu.

“Siku hizi hisia hiyo inajulikana kama msongo wa mawazo,” anasema Dkt Chaney.

“Lakini hisia hiyo zamani ilihusishwa na mgogoro wa kiimani kwa watu waliyoamua kufuata mkundo fulani wa maisha kwa kula kiapo cha uaminifu.”

2. Ghadhabu

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mtu akipandwa na ghadhabu inakuwa vigumu kwake kukaa kimya au kujituliza kwa mda huo

“Kwa maana nyingine hisia inayompata mtu akiwa na hasira,” anaelezea Dkt Chaney.

“Hali hii zamani ilikuwa rahisi kuidhibiti lakini siku hizi imekuwa vigumu.”

“Mtu aliyekabiliwa na ghadhabu huwa na hasira kupita kiasi. Huwa hawezi kujituliza mara nyingi huzungumza kwa hasira huku akrusha mikono na kutishia kufanya jambo baya ka yule aliyemkosea.

Lugha ambazo watu kama hawa wanatumia kuelezea hisia zao ilimaanisha kuwa walihisi vitu ambavyo hatuwezi kuvielezea,” anasema Dkt Chaney.

3. Masikitiko

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mwanamke aliye na masikitiko

Hii ni hisia inayompata mtu anapotatizwa na jambo fulani kisaikolojia.

“Zamani hali hiyo ilikuwa ikitafsiriwa kitofauti,” anasema Dkt Chaney.

Hadi karne ya 16, iliaminika kuwa afya ya mtu ilihusishwa na furaha aliyonayo moyoni na hali hiyo ilinekana kupitia tabasamu lake usoni

“Wakati mwingine watu wanaopatwa na hisia hiyo hufikwa na uwoga hata wakisikia kwa mfano kitu kikianguka,” anasema Dkt Chaney.

4. Kukumbuka mambo ya zamani

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Zamani hisia hii ilihusishwa na ugonjwa wa mabaharia au wahudumu wa meli katika karne ya 18.

Zamani hisia hii ilihusishwa na ugonjwa wa mabaharia au wahudumu wa meli katika karne ya 18.

“Tunatumia neno ‘nostalgia’ mara nyingi siku hizi, lakini neno hilo lilidhaniwa kuwa ugonjwa,”anasema Dkt Chaney.

Mabaharia zama hizo wakikabiliwa na hali ngumu safarini wanapatwa na hisia ya kukumbuka nyumbani.

Zama hizo mabaharia walikuwa wakionesha dalili za kuwa na uchovu mwilini.

Lakini zama hizi watu hukumbuka kwa mfano tamaduni nzuri za jadi au ujana wao kwa furaha.

5. Mshutuko baada ya shambulio

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mshtuko baada ya shambulio huwatatiza sana wanajeshi baada ya kutoka vitani

Watu wengi wameshawahi kupatwa na hisia hii lakini sana sana hisia hiyo zamani ilihusishwana wanajeshi waliyopigana vita vikuu vya kwanza vya dunia.

“Watu wanaopatwa na hisia hiyo mara nyingi hupoteza uwezo wa kusikia au mara nyingine hawaoneshi dalili za kuwa na matatizo yoyote,” anasema Dkt Chaney.

“Mwanzo wa vita, watu hao walidhani hali hiyo imetokana na wao kuwa karibu na milipuko iliyoathiri masikio yao. Lakini baadae iligunduliwa kuwa ni hisia ya mtu binafsi wakati huo.”

6. Hofu ya kupatwa na ugonjwa hatari

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mchoro wa mwanamume akimhudumia mwanamke aliyezimia

Katika karne ya 19 hisia kama hii ilihusishwa zaidi na msimamo wa mtu binafsi .

Huwezi kusikiliza tena

Baadhi ya dawa

“Inaaminiwa kuwa hisia hiyo ilitokana na hufu ya kupata maumivu makali katika mfumo neva ”Dkt Chaney.

Mtu anayepatwa na hisia hii hutatizika kiakili lakini ukimwangalia utadhani ni mzima hana neno.

7. Msimamo wa kimaadili

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mchoro wa jadi wa watu waliyokasirishwa na mtu aliyekiuka maadili

Neno hili “moral insanity” lilibuniwa na Dkt James Cowles Prichard mwaka 1835.

“Halina tafsiri nyingine zaidi ya maadili,” anasema Dkt Chaney.

“Hii ni kwa sababu kwa mda mrefu neneo hilo lilihisishwa zaidi na msimamo wa kisaikolojia

Kwa mfano haisia hii inaweza kumfanya mgonjwa kuonesha dalili za mtu mwenye tatizo la kiakili wakati vipimo halisi vinaonesha hana neno.

Tunaweza kusema kuwa ni hisia za watu wazima zilizopita maelezo .”

Unaweza pia kutizana:

Huwezi kusikiliza tena

Umuhimu wa afya ya uzazi kwa wanaumeSource link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *