Huduma Namba Kenya: Mahakama yaizuia serikali kwa kuhofia usalama wa taarifa binafsi


A Kenyan woman being registered for the Huduma Namba scheme in May last year

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

The government said it was mandatory to register for a Huduma Namba

Mahakama Kuu nchini Kenya imesitisha mpango tata wa utambulisho maalum unaofahamika kama Huduma Namba hadi pale sheria ya kulinda data ya watu binafsi itakapoanza kutekelezwa.

Maelezo binafsi kama vile, mahali unapoishi, kuchukuliwa kwa alama ya vidole na kazi mtu anayofanya, ilichukuliwa mwaka jana.

Wazo lilikuwa kusawazisha data ya mtu kama iliyohifadhiwa na serikali na kuiweka pamoja katika kitambulisho kimoja.

Jaji aliamua kwamba hatua hiyo inakiuka sheria kwa kila namna ikiwa maelezo ya watu binafsi hayatapewa ulinzi wa kutosha.

Sheria ya kulinda data iliyopitishwa mwezi Novemba mwaka 2019, italazimika kubuniwa katika tume itakayolinda taarifa binafsi za watu.

Lakini haijabainika tume hiyo itabuniwa lini na mkuu wake atateuliwa lini ili ianze kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi kutoka mji mkuu wa Nairobi.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Alama ya vidole ya mtu ilichukuliwa wakati wa usajili wa Huduma Namba mwaka uliopita

Hadi wakati huo mpango huo wa Hudma Namba, umesitishwa na jo0po la majaji watatu.

Majaji walisema nini?

Kwa kuwa taarifa zote muhimu za watu zitapatikana kwa kubofya kompyuta, walisema kwamba Wakenya wataathiriwa vibaya ikiwa maelezo hayo yatatumika vibaya.

Majajji pia waliamua kwamba ikiwa chembe chembe za vinasaba DNA, zitachukuliwa na kutumia GPS, mfumo wa kutambua nyumbani kwa mtu utakuwa ni kuingilia faragha yake na kuongeza kwamba hatua hiyo inakiuka katiba.

Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na Tume ya kitaifa kutetea haki za binadamu nchini Kenya (KNCHR), Tume ya Kenya ya kutetea haki za binadamu (KHRC), na kundi la kutetea haki ya jamii ya Wanubi nchini Kenya.

Jamii ya Wanubi ambayo imekuwa ikiishi katika mtaa wa Kibera- viungani mwa mji wa Nairobi- kwa zaidi ya karne moja, imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya kupata uraia wa Kenya kwa sababu waliletwa na utawala wa kikoloni wa Uingereza kutoka Sudan.

Hii inamaanisha watu wengi kutoka jamii hiyo hawakusajiliwa kupata Huduma Namba kwasababu wengi wao hawana vitambulisho vya kitaifa

Walikuwa wanataka mpango huo mzima ufutiliwe mbali kwasababu serikali inasema watu watahitajika kuwa na kitambulisho cha Huduma Namba kupata huduma katika ofisi za umma siku zijazo.

Uamuzi huu unaacha wapi hatima ya utambulisho wa kidijitali?

Kesi dhidi ya Huduma Namba inaangazia masuala yanayozunguka hofu ya watu wanaohofiwa kutengwa katika jamii na pia hatari inayozunguka suala zima la kuhifadhi data katika mfumo wa kidijitali.

Lakini wataalamu wa masuala ya kidijitali nchini Kenya wanasema ipo haja ya kutafakari kwa kina baadhi ya hoja zinazoibuliwa na mfumo huo wa utambulisho ambazo zimechangia kuwasilishwa kwa kesi ya kupinga mfumo huo hata kabla mpango wenyewe kuanza kutekelezwa.

”Tunahitaji kutathmini lengo halisi la mpango huo ni nini hasa- kuna”umuhimu gani” kuwa na kitambulisho cha Huduma”, alisema mmoja wa wachanganuzi wa masuala ya kisiasa nchini Kenya ambaye hakutaka kutambulishwa.

”Kwanini tunahitaji nambari moja maalum ya utambulisho? aliuza, ”Je kuna haja ya serikali kukusanya upya maelezo ambayo ilikuwa nayo tayari , kumtambulisha mwananchi wake?

Mtaalamu huyo pia aliaambia BBC kwamba ipo haja kuzingatia haki ya kimsingi hasa linapokuja suala la utambulisho.

Anasema juhudi za serikali kutaka kuwatambua wananchi wake kwa kutumia kitambulisho maalum haistahili kuwafanya watu kuhofia kutengwa katika jamii , kutumiwa vibaya au kuchunguzwa kisiri.

Mashirika ya kutetea haki nchini Kenya katika kesi iliyoamuliwa Ijumaa na mahakama kuu yaliangazia hatari na mpango huo na changamoto zinazotokana na mfumo wa utambulisho wa kidijitali.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *