Ipi hatma ya watu milioni 1.9 waliovuliwa urai India?


Watu milioni 4 walivuliwa uraia katika rasimu ya kwanza ya sajili ya kitaifa iliotolewa mwezi Julai mwaka huu

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Watu milioni 4 walivuliwa uraia katika rasimu ya kwanza ya sajili ya kitaifa iliotolewa mwezi Julai mwaka huu

India imechapisha orodha ya mwisho ya watu milioni 1.9 iliyowavua uraia wake Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Sajili ya kitaifa ya raia(NRC)ni orodha ya watu ambao wanaweza kuthibitisha kuwa waliinga nchini humo kufikia mwezi 24 Machi mwaka 1971, siku kabla ya Bangladesh kupata uhuru wake kutoka kwa Pakistan.

Watu ambao hawajajumuishwa katika sajili hiyo wana siku 120 kukata rufaa dhidi ya hatua ya kuvuliwa uraia wa nchi hiyo.

Haijabainika nini kitakachofuata baada ya hatua hiyo kutekelezwa.

India inasema mpango huo ni muhimu katika mchakato wa kuwabaini wahamiaji haramu kutoka Bangladesh.

Haki miliki ya picha
EPA

Image caption

NRC ilibuniwa mwaka 1951 kutofautisha mzaliwa wa Assam ambaye ni raia halisi na mhamiaji kutoka taifa jirani la Bangladesh.

Tayari maelfu ya watuwaliokamatwa wanazuiliwa katika kambi ya muda kwa kushukiwa kuwa raia wa kigeni, lakini kuna hofu ikiwa watakubalika walikotoka.

Mpango huo umezua gumzo kali baadhi ya watu wakidai ni”hujuma” dhidi ya jamii ya Assam walio wachache.

Rasimu ya sajili hiyo iliyochapishwa mwaka jana iliwatenga watu milioni nne.

Sajili ya Kitaifa ya raia ni nini?

Sajili ya NRC ilibuniwa mwaka 1951 to kutofautisha mzaliwa wa Assam ambaye ni raia halisi na mhamiaji kutoka taifa jirani la Bangladesh.

Sajili hiyo imefanyiwa mabadiliko kwa mara ya kwanza.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Saheb Ali, 55, mkazi wa Wilaya ya Goalpara amevuliwa uraia

Familia katika jimbo la Assam wamekuwa wakitakiwa kuwasilisha stakabadhi zinazo thibitisha kuwa ni wazawa wa nchi hiyo huku wale wanaoshindwa kufanya hivyo wakichukuliwa kuwa wahamiaji haramu

Chama cha Bharatiya Janata Party (BJP) cha Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, kwa muda mrefu kimekuwa kikipinga uhamiaji haramu nchini humo lakini miaka ya hivi karibuni kimeipatia kipaaumbelea sajili ya kitaifa ya raia NRC.

Kwa nini sajili hiyo inatumika Assam?

Assam ni moja ya majimbo ya India inayokaliwa na watu kutoka jamii tofauti na suala la uraia wao limekuwa likitiliwa shaka kwamuda mrefu.

Miongoni mwa watu hao ni jamii ya Bengali na Assamese-wanaozungumza kihindi.

Thuluthi tatu ya watu milioni 32 million wanaoishi katika jimbo hilo ni Waislamu, idadi ambayo ni yapili kwa ukubwa baada ya wale wanaoishi Kashmir.

Wengi wao wametokana na kizazi cha wahamiaji walikalia eneo hilo wakati wa utawala wa Uingereza.

Lakini wahamiaji haramu kutoka taifa jirani la Bangladesh, ni kilomita 4,000- kutoka mpaka wa India, wamekuwa wakuwa wakiishi kwa hofu kwa miongo kadhaa sasa.

Mwaka 2016 serikali ilitangaza kuwa inakadiria karibu watu milioni 20 wanaoishi India ni wahamiaji haramu..

Watu hao 1.9 watatambuliwa lini hawana nchi?

Watu ambao majina yao hayapo katika sajo ya kitaifa wanaweza kukata rufaa katika mahakama maalum iliyobuniwa kusikiliza kesi yao.

Pia wanaweza kuwasilisha kesi katika mahakama kuu au Mahakama ya Juu zaidi.

Kuna hofu rufaa hizo zitachukua muda mrefu kuamuliwa hali ambayo itasababisha msongamano zaidi mahakamani huku familia masikini zikikabiliwan a wakati mgumu kutafuta fedha za kupigana kisheri kuhusu kesi ya uraia wao.

Watu watakaopoteza rufaa waliowasilisha huenda wakafungwa jela.

Haki miliki ya picha
Citizens for Justice and Peace

Image caption

Baba na mwanawe waliwahi kujitoa uhai kutokana na suala la uraia wao

Watu 1,000 waliothibitishwa kuwa raia wa kigeni wamekuwa wakizuiliwa kwa miezi sita sasa katika jela za India.

Serikali ya Nerendra Modi pia inajenga jela mpya itakayoweza kuwa na uwezo wa kuwazuilia hadi watu 3000.

“Watu ambao majina yao hayapo katika sajili ya uraia wamekuwa wakiishi kwa hofu wasijue hatma yao ni ipi,” Sangeeta Barooah Pisharoty, mwandishi wa Assam wa kitabu: The Accord, The Discord, aliiambia BBC

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Hatua ya kuvuliwa uraia kwa watu hao inatarajiwa kusababisha maandamano kmakubwaSource link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *