Je ni kweli kuwa baadhi ya kazi uongo unasaidia?


Utafiti umeonyesha kuwa katika baadhi ya kazi, wafanyakazi wanaodanganya wawapo kazini huaminiwa kuliko wanaosema ukweli

Haki miliki ya picha
Alamy Stock Photo

Image caption

Utafiti umeonyesha kuwa katika baadhi ya kazi, wafanyakazi wanaodanganya wawapo kazini huaminiwa kuliko wanaosema ukweli

Wengi wanakiri kuwa wana la kuungama. kwani wamedanganya sana. Katika kuanzisha au kusitisha gumzo, mara nyingine hata kuepuka kuumiza hisia za wenzao na hata zao binafsi katika maisha ya kawaida ya kijamii na kikazi kwa njia nyingi mbali mbali.

Kwa kiasi fulani tunafahamu kuwa watu tunaofanya nao kazi wanatudanganya. hawawezi kuwa kila siku siku yao ni nzuri, wanafurahia kazi na kuwa wenye kufurahia wenzao wanapopandishwa vyeo badala yao.

Lakini ni vipi kudanganya kunapokuwasi tu kwa ajili ya hisia , lakini inapokuwa ni kwa ajili ya kazi? Utafiti mpya unaonyesha kuwa sababu moja inayosababisha uongo kuimarika miongoni mwa watu wa taaluma fulani wenye mitizamo ya kubadilika ni kwamba watu hao ni wazuri kwa kazi zao.

Mitizamo juu ya uongo katika sehemu za kazi

Kwa ujumla, hisia za kudanganywa katika maeneo ya kazi hutazamwa kwa mtizamo hasi – kama watu watapatikana kuwa waongo huenda likawa si jambo zuri kwa kazi zao . Na uongo unaweza kuwa sumu kwa utamaduni wa imani na kufanya kazi kwa pamoja.

Lakini kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni wa wanazuoni wa Kimarekani Brian C Gunia na Emma E Levine, kuna kazi za kipekee ambazo zinachukuliwa kuwa ni za mauzo ya hali ya juu zaidi ya zinazowahusu wateja zinazotumia uongo zaidi ili kupata mafanikio.

Haki miliki ya picha
Alamy Stock Photo

Image caption

Kazi za kunadimasoko ya biashara ni moja wapo ya kazi zilizotajwa kuhusisha uongo ili kupata mafanikio ya kibiashara

Utafiti mmoja ulibaini kuwa watu wanamini kuwa wale wanosema uongo zaidi ndio wanaofanya kazi kwa ubora zaidi.

Katika utafiti mmoja kuhusu masoko , kazi zinazohusiana na wateja kile kinachohitajika ni kuridhisha haja za mteja za kununua bidhaa , huku kazi zinazohusu mauzi hulenga kufikia malengo ya muuzaji mwenyewe.

Watafiti Gunia na Levine waliwauliza washiriki wa utafiti – ambao walijumuisha wanafunzi wa masomo ya biashara na watafiti mtandao w amauzo wa Amazon wa Marekani – kuorodhesha kazi fulani kulingana na namna wanavyoziona kuwa za mauzo na wazipe viwango wakiambatanisha na watu binafsi kulingana na uwezo wao wa kikazi.

Washiriki walipewa mfano wa mazingira kama ifuatavyo : Unapopanga matumizi “julie”anadai kwamba kuendesha teksi ni gharama kubwa zaidi ya ilivyo ; “James” anajifanya kuwa anafiurahia kuendesha meli kwenda pamoja na bosi mwenye ari.

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena

Je, rushwa katika soko la ajira Tanzania imekuathiri?

Matokeo yake , waliojibu waliamini kuwa watu walioonyesha kuwa ni waongo wangekuwa na mafanikio zaidi katika mauzo ya kazi za mauzo na wangeweza kupewa kipaumbele katika ajira. Kwa mfano, 84% ya washiriki walichagua kuwaajiri waongo kwa kazi za juu katika kazi ya ubaharia , huku 75% wakichagua kuwaajiri watu wasio waongo kwa sekta za kazi za chini za mauzo.

Watu wanaamini kuwa watu binafsi ambao wanaweza kudhibiti hisia zao wana uwezo mkubwa zaidi ya wale ambao hawawezi kufanya hivyo, anasema Levine.

Katika Utafiti wa hivi karibuni juu ya uhusiano kati ya mtizamo wa uongo na mtizamo wa uwezo “tuliwaajiri makusudi wanafunzi wa biashara ili tuwe na uhakika wa unyanyapaa, tuliwachunguza wafanyabiashara wajao “, anaeleza Levine, wa Chuo cha mafunzo ya biashara cha Chicago . Wanafunzi wanaolenga kupata kazi za utawala “wanaweza kuamini kuwa ni kweli uongo ni ishara ya uwezo katika kazi hizi na hivyo ni bora kuingiza imani hizi watu wanapowaajiri watu katika siku zijazo “.

Haki miliki ya picha
Alamy Stock Photo

Image caption

Kwa mfano baadhi ya kazi kwa mfano wafanyakazi wanatarajiwa kutumia udanganyifu kuwaficha wachunguzi wa siri

Je kuna faida ya kudanganya kazini ?

Uongo unaweza kuwa hata ni mkakati wa kampuni nzima ,kama vile kituo cha kupokea simu cha kampuni kuwaagiza wafanyakazi kunafanyia kazi katika nchi nyingine tofauti kulingana na vile ambavyo wateja wanataka kusikia.

Baadhi ya kazi zinahitaji utendaji unaostahili au huduma ambazo ni ghusi na za kukanganya. Kama asemavyo Levine , “watu wanamini kwamba watu binafsi ambao wanaweza kudhibiti hisia zaowana uwezo wa kikazi kuliko wale ambao hawawezi “. Kuonyesha hisia mahali pasipotakikana ni tabia ambayo si ya busara.

Huwezi kusikiliza tena

Haba na Haba: Una mkataba wa ajira pahala unapofanyia kazi?

Hii inaweza kuwa ukweli hususan kwa watu wenye ushawishi kwenye mitandao ya kijamii ambao huficha maneno kwenye sentensi kati ya ukweli na lugha ya mauzo. Nyota wa Instagram ambao huweka taarifa za gushi za “kushtukiza ” kushika uchumba kwa mfano, licha ya kwamba hii inaweza kuwaathiri pale uongo unapojulikana.

Uongo mdogomdogo unaofurahisha

Wakati mwingine faida za uongo zinaonekana hata kuwa chaguo la kimaadili . “katika utafiti wangu, ninapata kuwa watu wengi huwa wanaafiki na kupenda uongo ambao unaelezwa kwa ajili ya kuwafaidi “, amasema. Kwa mfano, “Waajiriwa wanaamini kuwa wafanyakazi wenzao wanafaa kuwapa wenzao mrejesho ambao hawawezi kuutekeleza ambao utanusuru tu hisia zao. Na wagonjwa wa saratani hufurahia majibu ya uongo yenye kuwapa matumaini zaidi ya ukweli kuhusu saratani “.

Kunaweza kuwa na ushawishi wa kitamaduni kwa mtizamo wa aina hii, kama baadhi ya tafiti zinazvyosema kutoka kwa mtizamo wa jumla wa tamaduni kuwa kusema uongo inafaa ili kulinda sura na amani ya kikundi au jamii.

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena

Haba na Haba: Unawajibikaje kuongeza ajira kwa vijana Tanzania?

Utafiti mmoja ulioandikwa na mmoja wa watafiti Michele Gelfand, mwanasaikolojia katika Chuo kikuu cha Maryland,uliwahusisha wanafunzi zaidi ya 1,500 kutoka nchi 15 katika shughuli ya mazungumzo ya kibiashatra ambayo udanganyifu ungesaidia kibiashara.

Wale waliokiuwa katika kikundi kama vile nchi za Korea kusini na Ugiriki walitumia udanganyifu kuliko wanafunzi waliokuwa binafsi(mmoja mmoja) wanaotoka katika nchi za kama vile Australia na Ujerumani), licha ya kwamba udanganyifu ulikuwa ni wa kiwango cha juu kwa ujumla.

Uongo mdogo huwa si sumu kila wakati. Lakini kwa ujumla , maeneo ya kazi watu watafanya kazi kwa ufanisi zaidi ikiwa watahisi kuwa wamewezeshwa kutegemea ukweli.

Wanasiasa fulani maarufu ni mfano mzuri wa matokeo ya athari mbaya na kubwa pamoja na mgawanyiko vinavyotokea kwa kazi ya mtu.

Kwa hiyo ufanya udanganyifu mdogo unaokufanya uwe mzuri zaidi katika kazi yako? Huenda si jambo linalofaa. Wanasema wataalamu.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *