Je ni kweli mtu hupata hisia tofauti inapofika siku ya Ijumaa


Mhariri wa BBC Idhaa ya Kiswahili anasema IJumaa ni siku ambayo hujisikia mwepesi

Image caption

Mhariri wa BBC Idhaa ya Kiswahili anasema IJumaa ni siku ambayo hujisikia mwepesi

Kumekuwa na hisia za muda mrefu miongoni mwa jamii na watu mbali mbali duniani kwamba siku ya Ijumaa ni siku ya Furaha. Baadhi wamediriki hata kuiita ”Furahi day”

Hii hutokana na fikra za watu kwamba Ijumaa ni siku ya mwisho ya kazi katika ofisi nyingi hususani za serikali na hivyo kunakuwa na hisia kwamba baada ya Ijumaa wengi huenda mapumzikoni siku inayofuata yaani Jumamosi na pia Jumapili.

Mara nyingi utawasikia watu wakisema, siamini leo ni Ijumaa!.

Japo Ijumaa si siku ya mapumziko kwa kila mtu, umekuwa ni utamaduni wa watu kuiona siku hii kama siku njema.

Ijumaa ni siku ambayo baadhi wamekuwa wakiiona kuwa ni bora kuliko Jumatatu kwasababu Jumatatu ni siku ya kuanza kazi na pilka pilka nyingine nyingi za kimaisha na mwanzo wa wiki ya kazi.

”Kwangu mimi siku ya Ijumaa kama hivi leo sio siku ya mbio mbio, najiskia mwepesi, najitayarisha natazamia wikendi Jumamosi na Jumapili. Ndio mana kama siku ya leo sikuvaa kirasmi, yani angalau nijiskie kwamba nimeanza wikendi”Anasema mhariri wa BBC Odhiambo Joseph ambaye alikuwa katika Ofisi za BBC mjini Nairobi akielekea kwenye mkutano wa kazi wa siku.

Na kutokana na hisia za Siku ya Ujumaa kwenye mitandao ya kijamii baadhi ya watu na makundi huanzisha gumzo kuelezea ni vipi wanavyohisi katika siku ya Ijumaa. Tom Hall kwenye ukurasa wa Twitter chini ya Hashtag #FridayFeeling amekuwa na hisia mchanganyiko:

Chini ya #FridayFeeling …tarehe 31 Mei 2019 watu mbali mbali duniani wamekuwa wakielezea hisia walizonazo katika siku ya Ijumaa:

Kwamba Unaweza kuhisi ni Ijumaa ndani ya mifupa yako kama hivi:

Hata hivyo wataalamu wa masuala ya kijamii wanasema kuwa hakuna tofauti kati ya siku ya Ijumaa na siku nyingine na kwamba ni mtizamo tu wa mtu binafsi na jamii kuhisi kwamba siku moja na siku nyingine zina utofauti.

Mfano kwa wale ambao wanaiona siku ya Jumatatu kuwa ni siku isiyofurahisha wanashauriwa kuichukulia kama siku njema na ikiwezekana kwa wale wanaofanya kazi Jumatatu wapange mipango yao ya kazi mapema na kuvaa nguo ambazo wangepena kuzivaa Ijumaa kama vile viatu vya wazi , jinzi na tisheti, iwapo sio lazima kuvaa nguo rasmi kazini ili wahisi Jumatatu kama Ijumaa.

Wanasema siku za Jumatatu hadi Alhamisi zinaweza pia kuwa siku za raha pia.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *