Je, uchumi wa Zimbabwe sasa uko kwenye hali mbaya zaidi ya wakati wa utawala wa Mugabe?


Quote card

Madai: Maisha ya Zimbabwe sasa ni magumu zaidi hata yalivyokuwa wakati wa utawala wa Robert Mugabe, hiyo ni kwa mujibu wa Fadzayi Mahere wa chama cha upinzani cha MDC.

Je madai haya yana ukweli wowote kuwa miezi ya hivi karibuni uchumi umekuwa mbaya zaidi?

Kwa sababu hata wakati wa uongozi wa Mugabe kuna kipindi hali ya kiuchumi ilikuwa mbaya zaidi.

Zimbabweans protest against the government's handling of the economy

Haki miliki ya picha
Getty Images

Presentational grey line

Upande wa upinzani nchini Zimbabwe umewataka watu waandamane juu ya hali mbaya ya kiuchumi katika taifa hilo, serikali imeshutumiwa kwa kushindwa kufanya kazi yake.

Tangu mwaka 2017, Zimbabwe imekuwa chini ya utawala wa rais Emmerson Mnangagwa, baada ya jeshi kumuondoa kwa Robert Mugabe baada ya kutawala kwa kipindi cha muda mrefu .

Tumepima utofauti huo kwa kuangalia viashiria vya uchumi vya taifa vya maisha ya raia wa Zimbabwe kuwa wako kwenye hali mbaya sasa zaidi ya walivyokuwa kabla ya Mnangagwa kuingia madarakani.

Hii inaweza kuchukuliwa kama ufinyu wa ajira na mishahara kwani biashara imekuwa ya mashindano katika nyakati ngumu za kiuchumi.

Licha ya takwimu iliyokadiriwa ya mwaka 2019 iko chini kidogo ya ile ya 2017, amabayo ndio ilikuwa mwaka wa mwisho madarakani wa raisi Mugabe.

Pamoja na kuwa raia wa Zimbabwe wanaweza kuwa wanakabiliana na changamoto ya kushuka kwa takwimu hiyo ya hivi karibuni, si rahisi kujadili takwimu kutokana na hali kuwa mbaya zaidi hivi leo kuliko ya uongozi uliopita.

Hata hivyo, hatua nyingine muhimu haina budi kuchukuliwa juu ya hali ya uchumi ambayo ni hatua nyingine ya uwekezaji katika biashara.

Uchumi umeshuka kwa kasi tangu mwaka 2017. Ambapo katika asilimia ya thamani ya uchumi, ilikuwa takribani mara tatu juu zaidi ya takwimu iliyokadiriwa ya mwaka 2019.

Serikali ya Zimbabwe bado inalaumu vikwazo vya kimataifa ambavyo vimekuwepo tangu mwaka 2002 vikiharibu uchumi wa nchi hiyo.

Hivi vikwazo vimekuwa vikilenga maafisa wa ngazi za juu na wenye makampuni, huku Marekani ikisema haitaiondolewa vikwazo Zimbabwe mpaka pale itakapooona mabadiliko ya kisiasa mbadala nchini humo.

Raia wa Zimbabwe wamekuwa na mtazamo tofauti juu ya hali ya uchumi nchini humo, huku mfumko wa bei ukiwa unawaathiri maisha yao ya kila siku kuliko ukuaji wa jumla au uwekezaji wa takwimu.

Mwishoni mwa mwaka 2017 ambapo Mugabe aliondolewa madarakani, kiwango cha mwaka cha mfumuko wa bei ambacho ni kiwango cha kupanda bei takribani asilimia 5.

Mfumuko wa bei umebaki chini mpaka kuelekea mwishoni mwa mwaka 2018, lakini imepanda kwa kasi mwanzoni mwa nusu mwaka 2019, kufikia kiwango cha mwaka cha asilimia 176 mwezi Juni.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Foleni katika ATM za benki mjini Harare

Hiki ni kipimo cha bei ya jumla ya watumiaji katika uchumi.

Kama hali hii haitazingatiwa katika bei za chakula, basi hali itazidi kuwa ngumu.

Takwimu zilizotolewa na Umoja wa Mataifa ya mfumuko wa bei za vyakula ya mwaka iliyotolewa mwezi Juni mwaka 2019 ilipimwa huku ikionesha kupanda na kufikia asilimia 250.

Hivyo gharama za vyakula katika masoko imeongezeka, huku upatikanaji wa mafuta ukiwa mdogo na pensheni za watu kuwa hazina thamani hivi sasa.

Shirika la chakula duniani (WFO) limeomba ufadhili wa chakula , kwa kile kinachosemwa kuwa ‘janga kubwa la njaa’

Inasemekana kuwa watu wa Zimbabwe waliathirika kwa kiasi kikubwa na kimbunga cha Idai walichokabiliana nacho mwezi Machi, huku ukame ukiathiri baadhi ya sehemu za nchi hiyo na kupelekea ‘uchumi kushuka’

Serikali ya nchi hiyo imeanzisha pesa mpya ya nchi hiyo baada ya takribani kumi ya kutegemea pesa ya Kimarekani.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Hatua hii imesababisha kilio kwa wafanyakazi wengi ambao walipendelea kulipwa kwa dola za Kimarekani, ambao mishahara yao imeshuka kwa mwaka uliopita kutokana na mfumuko huo wa bei.

Je hali nchini Zimbabwe itazidi kuwa mbaya?

Licha ya hali mbaya ya kiuchumi hivi sasa, hali ilikuwa ngumu zaidi katika utawala wa uongozi uliopita wa Mugabe.

Mwaka 2007-09, nchi ya Zimbabwe ilipitia kipindi kigumu cha uchumi kuyumba kutokana na kupanda kwa mfumuko wa bei na kufanya thamani ya pesa ya nchi hiyo kuwa ndogo kulinganisha na miaka mingine.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinasema katika kipindi cha mwaka 2008, kiwango cha mfumuko wa bei kilikuwa juu ya bilioni 500 asilimia , na kulikuwa na ukosefu wa ajira.

“Mnamo mwaka 2008, kulikuwa na uhaba wa chakula. Hali ilikuwa ngumu zaidi shambani kuliko hivi sasa’, anasema mwandishi wa BBC Shingai Nyoka kutoka Harare.

Kulikuwa na kuenea kwa machafuko na mgawanyo wa serikali ambapo raia wengi waliuawa na kukamatwa na jeshi la polisi nchini humo.

‘Bw Mugabe ameacha uchumi mzuri wa utendaji ambapo katika miaka 15 ya mwanzo ya utawala wake alioujenga, umeunda madarasa ya watu wa kati’, alisema Bi Nyoka

‘Lakini miaka 20 ya utawala wake umeharibu uchumi. Katika miaka miwili ya ofisini, serikali iliyopo hivi sasa bado inajaribu kutatua matatizo yaliyoachwa na utawala wa Mugabe.’

Je, Serikali inasemaje?

Haki miliki ya picha
Getty Images

Tangu serikali mpya imeingia madarakani imefanya ustadi wa vipimo- kupunguza matumizi, kupunguza baadhi ya mishahara kutoka sekta za umma na kuleta kodi mpya ambayo itarejesha uchumi kuwa imara.

Imesema mabadiliko ni muhimu katika kujenga mazingira rafiki kwa wawekezaji ili waweze kuleta ajira kwa wananchi.

Mtaalamu wa uchumi kutoka Zimbabwe, Godfrey Kanyenze amesema serikali ya sasa imeziweka sera za nchi hiyo katika ufanyaji kazi wake , hivyo kutoa sugu ya mfumuko wa bei na umaskini wa walio wengi katika nchi hiyo.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *