Jinsi wanawake wa Mexico wanavyotumiwa kingono na wafanyabiashara ya madawa ya kulevya Mexico


Mwnamke

Chanzo cha picha, Getty Images

Jimbo la magharibi mwa Mexico la Sinaloa ni makao ya magenge hatari na sugu ya wauzaji wa mihadarati nchini humo. Pesa inayopatikana kutokana na mihadarati imeacha chapa yake kwenye mahusiano baina ya wafanyabiashara wa mihadarati na wanawake vijana-na kuchochea kiu ya kufanyiwa upasuaji wa kubadilisha maumbile vijana (plastic surgery).

Kwenye dawati lake la kliniki katika mji mkuu Culiacan, dokta Rafaela Martinez Terrazas huketi kila siku kupokea wateja wanawake wanaotaka kufanyikwa upasuaji unaohusiana na kile kinachofahamika kama “narco-aesthetic”.

“Kiuno chembembe … nyonga pana na makalio makubwa … Na kama ni kama ni upasuaji wa matiti wote hutaka yawe makubwa ,” anasema Martinez.

Mwanamke mwenye umbile hili la ”namba nane” mara nyingi hufahamika kama buchona nchini Mexico – hususan kama anajua kuvaa mavazi na vipuli vya kuvutia kuvutia na vya bei kali vilivyotengenezwa na nembo maarufu za mavazi na vipodozi, mwenye mpenzi ambaye ni mlanguzi wa mihadarati.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *