Kenya imepanga kupiga marufuku mahusiano ya kimapenzi miongoni mwa maafisa wa polisi.


polisi

Chanzo cha picha, AFP

Hatua hii ina nia ya kupunguza viwango vya uhalifu unaotokana na masuala ya mapenzi miongoni mwa maafisa hao, Waziri wa usalama wa Ndani alieleza hayo kwenye sherehe katika chuo kimoja cha polisi nchini humo.

Kanuni hizo kwanza zinahitaji kupewa idhini na Baraza la Usalama la Taifa, linalosimamia vikosi vyote vya usalama vya nchi hiyo, Fred Matiang’i alisema.

Ndani ya huduma ya polisi , mahusiano yalishapigwa marufuku miongoni mwa maafisa wa vyeo tofauti, alieleza.

Miezi michache iliyopita, kulikuwa na ongezeko la mauaji ya wapenzi, waziri huyo alieleza.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *