Kenyatta ndiye mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika MasharikiHii ni kufuatia mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao uliohudhuriwa na viongozi wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

Dkt Peter Mathuki, raia wa Kenya, sasa ndiye katibu mkuu mpya wa Jumuiya hiyo, akichukua nafasi ya Balozi Liberate Mfumukeko, raia wa Burundi, ambaye amekalisha muhula wake.

Kabla ya uteuzi huo, Mathuki alikuwa mkurugenzi mtendaji wa baraza la Biashara la nchi za Afrika mashariki.

Kwenye mkutano huo, ambao pia ulihudhuriwa na rais Paul Kagame wa Rwanda na makamu rais wa Tanzania tanzania Samia Suluhu Hassan, viongozi wa nchi wanachama walisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiano. Kwenye hafla ya Jumamosi, mmoja wa majaji wapya wa mahakama ya haki ya Afrika Mashariki, Kathurima M’Inoti pia aliapishwa.

Imetayarishwa na Asiraji Mvungi, Arusha, TanzaniaSource link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *