Kifafa: Ugonjwa wa ajabu wa Afrika Mashariki


Msichana aliyeungua kwa moto

Haki miliki ya picha
Provision Charitable Foundation

Image caption

Watu wenye dalili za kifafa mara nyingi huungua na kupta majeraha mengine kutokana na kuanguka wanapopika ama kuangukia vitu vingine vya kuumiza

Kabila hili huishi kwenye maeneo ya nyanda za juu ya Mahenge nchini Tanzania: Eneo hilo limezingirwa na milima, kat kati ya misitu.

Wameweza kuishi eneo hilo lililojitenga kwa miaka mingi , na kuendelea na maisha yao ya ukimya ambayo na kujitenga na kwa kiwango kikubwa kutotambuliwa maeneo mengine ya dunia

Lakini mambo yalibadilika pale daktari mmoja raia wa Norway alipowasili kwenye eneo lao mwaka 1959.

Warembo wazusha mshangao bungeni Uganda

Louise Jilek-Aall alikuwa na umri wa miaka 28 tu, alipowasili huko baada ya kuhitimu shule ya mafunzo ya matibabuna kuamua kuanzisha kliniki kwenye eneo hilo.

Lakini mara tu baada ya kuanza kazi yake alibaini kitu fulani cha ajabu ambacho hakukitarajia.

Karibu kila siku, watoto wadogo wenye umri wa hadi miaka miwili walianza kufika kwenye ofisi yake wakiwa na majeraha makubwa ya kuungua.

Katika tukio moja, mtoto mmoja wa kike aliletwa hospitalini ameungua kiasi cha kutoweza kutambuliwa ; wengine wengi walikufa kutokana na majeraha.

Haki miliki ya picha
Provision Charitable Foundation

Image caption

Louise Jilek-Aall, pichani (kushoto) mwaka 2009, aliushughulikia sana ugonjwa kifafa

Mara kwa mara makovu yalikua na utando wenye rangi ya waridi iliyopauka, iliyofunika eneo hilo la mwili miaka mingi kutokana na majeraha.

Na hali hii ilijitokeza hasa kwa vijana wadogo na ungedhani kuwa walipata ajali tofauti.

Hatimaye Uingereza yawaruhusu wazazi kumpa mtoto bangi kama tiba

Wakati Jilek-Aall alipojaribu kubaini ni nini kilichowakuwa kinaendelea alikabiliwa na uoga na kutengwa.

Hata ndugu wa watoto walikataa kabisa kuelezea hali hiyo ya kutisha.

Hatimae Jilek-Aall alibaini kwamba wagonjwa wake walikuwa na ugonjwa waliouita kifafa – neno la Kiswahili linalomaanisha ”kifo kidogo” – unaowawafanya waanguke.

Wakati mwingine huwafanya waanguke ardhini wanapokuwa wanapika chakula chao. Wakati mwingine huanguka ndani ya mto.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Ugonjwa wa kifafa wakati mmoja ulifikiriwa kuwa unasababishwa na minyoo aina ya kupe inayosababisha upofu

Jambo jingine lla kushangaza ni kwamba watoto hao hao pia walidumaa, kutokuwa na uwezo wa kiakili na walikuwa na tabia na sura zisizo za kawaida kama vile uso wa kushangaa wanapomtazama mtu au vitu na kwa muda mrefu.

Lil Wayne alazwa hospitalini kwa kuugua kifafa

Kile kilichoshangaza zaidi ni namna walivyokuwa “wakionyesha ishara ya kukubali kwa kichwa “; mara kadhaa kwa siku, kufunga macho na kuangusha vichwa vyao vifuani .

Waliishi na ugonjwa huo kwa miaka kadhaa na hatimae kufa kifo cha mapema.

Ingawa kila mtu wa kabila la wapogoro aliuogopa ugonjwa kifafa sana, maradhi hayo yalikuwa hayajawahi kusikika katika maeneo mengine nchini.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Baadae ugonjwa wa kifafa ulibainika katika maeneo ya Sudan Kusini na kaskazini mwa Uganda

Hata makabila mengine jirani hayakuwahi kuusikia ugonjwa huo.

Baadae maradhi ya kifafa yalibainika kwenye maeneo mengine ya Afrika masharika, kuanzia Sudan Kusini hadi Kaskazini mwa Uganda ambako umeathiri maisha ya maelfu ya watu.Katika eneo jipya hujitokeza kama mlipuko.

Ni nini hasa kinachosababisha kifafa? Na ni vipi kinaweza kusitishwa?.

Hadi leo, hakuna anayejua kinachosababisha maradhi ya kifafa.

Miaka ya nyuma, ugonjwa huo ulikubalika kama aina fulani ya ukoma inayojitokeza kwa nadra sana.

Lakini sasa uchunguzi wa hivi karibuni umedokeza kuwa huenda ukawa ni ugonjwa unaosababishwa na kuathirika kwa ubongo, unaojitokeza kama mchanganyiko wa kifafa na baadhi ya dalili za ugonjwa wa kudorora kwa ubongo.

Mwishowe ni waathirika ambao kupata madhara yake kama vile kuharibika kwa ubongo na ajali, ali afya duni ya akili na kutelekezwa

Kile tunachokifahamu hadi sasa juu ya kifafa?

Kuna nadharia nyingi za kufikirika kuhusu kifafa. Katika eneo la Mahenge, wenyeji wanakihusisha kifafa na kiashiria cha tukio au jambo baya litakalotokea siku zijazo ambapo hujitakasa kwa kujimwagia maji kwenye mabega yao, na kuvuta harufu . Halafu hufungua macho ya na maji hubadilika kuwa mekundu.

Jambo la wazi ni kwamba si ugonjwa wa kurithi . “Japo huwa unatokea miongoni mwa familia, huu ni ugonjwa unaoweza kujitokeza na kupotea ,” anasema Peter Spencer, mtaalamu wa magonjwa ya ubongo katika taasisi ya Oregon Institute of Occupational Health Sciences. “ulijitokeza kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1997 kaskazini mwa Uganda, ukawakumba watu wengi na baadae ukatoweka miaka ya 2000 . Huwezi kuuelezea kama ugonjwa wa urithi , kwasababu huwezi sivyo ulivyo .”

Kwa sasa, chanzo cha ugonjwa huo kimebakia kuwa kisichofahamika.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *