Kifo cha George Floyd: Maandamano yafanyika miji tofauti Marekani licha tahadhari ya kutotoka nje kutangazwa.


Huwezi kusikiliza tena

Waandamanaji waliingia mitaani kuelezea hasira yao kufuatia kifo cha George Floyd

Amri ya kutotoka nje imetangazwa katika miji kadhaa nchi Marekani, kukabiliana na ghasia zilizosababishwa na kilo cha mtu mweusi aliyekamatwa na polisi.

Amri ya kutotoka nje imetangazwa katika miji tofauti nchi Marekani kukabiliana na ghasia zilizosababishwa na kilo cha mtu mweusi aliyekamatwa na polisi.

Lakini amri hilo imepuuzwa katika maeneo mengi, huku maduka yakiibiwa, magari yakichomwa moto na majengo yakiharibiwa. Polisi wa kukabiliana na ghasia wamekuwa wakitumia vitoa machozi na risasi za milita kuwatawanya waandamanaji.

Rais Trump ametoa wito wa “utulivu” kufuatia kifo cha George Floyd, laking amesema hataruhusu magenge ya wahalifu kutumia kifo hicho kutekeleza vitendo vya uhalifu.

Afisa aliyehusika na kifo hicho ambaye tayari amefutwa kazi ameshitakiwa kwa mauaji ya Bw. Floyd, aliyekuwa na umri wa miaka 46, mjini Minneapolis.

Derek Chauvin, 44, anatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Jumatatu.

Bw. Chauvin alionekana katika kanda ya video akipiga goti kwenye shingo la Floyd kwa dakika kadhaa huku Floyd akisikika akisema kuwa hawezi kupumua.

Maafisa wengine watatu waliokuwepo wakati wa tukio hilo pia wamefutwa kazi.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Fataki zililipuka karibu na mstari wa polisi wakati wa maandamano Atlanta

Tukio la Floyd limeibua ghadhabu miongoni mwa Wamarekani juu ya mauaji yanayotekelezwa na polisi dhidi ya watu weusi.

Hii inafuatia kesi maarufu ya mauaji ya Michael Brown mjini Ferguson, Eric Garner mjini New York na kesi nyingine zilizowasilishwa mahakamani na vugu vugu linalojulikana kama Black Lives Matters.

Lakini kwa wengine mauaji hayo yametoa nafasi ya kuangazia kwa unadani kadhia ya ubaguzi na kutengwa kwa jamii ya weusi, hali ambayo imeshuhudiwa kwa miaka mingi, sio tu mjini Minneapolis pekee.

Nini kinachofanyika katika maandamano ya sasa?

Maandamano makubwa yamefanyika katika karibu miji 30 nchini Marekani. Yalikuwa ya amani siku ya Jumamosi, lakini baadae yaliguka kuwa ya vurugu.

Mji wa Los Angeles ulioathiriwa zaidi na ghasia hizo. Gavana wa Jimbo la California, Gavin Newsom alitangaza hali ya hatari katika mji huo na kuagiza kupelekwa kwa walinzi wa kitaifa- kikosi maalum cha wanajeshi wa kukabilianna na ghasia za ndani ya nchi.

Mji huo umewekwa chini y amir ya kutotoka nje kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi na moja unusu asubuhi. Maduka kadhaa yameibiwa, yakiwemo maduka maarufu ya, Melrose na Fairfax, huku kanda za videozonaswa kutoka angani zikionesha baadhi ya majengo yakiteketea baaada ya kuchomwa motoyakiwaka moto. Mamie ya watt wamekamtwa kwa kukiuka agio la ktotoka nje.

Maya Eric Garcetti amaesema hizi ni “vurugu mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa” tangu maandamano ya mwaka 1992 ambayo yalisababishwa na kuondolewa mashitaka polisi katika kichapo cha Rodney King.

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Polisi wamesambazwa mitaani huku mioto ikiwaka katika Los Angeles, ambayo imewekwa katika hali ya tahadhari ya kutotoka nje

Hakujaripotiwa ghasia usiku kucha mjini Minneapolis, ambako George Floyd aliuawa. Maafisa 700 wa ulinzi wa kitaifa wanaongoza shughuli ya kuhakikisha amri ya kutotoka nje inazingatiwa. Gazeti la Star Tribune linaripoti kuwa hali imetulia katika mji huo ikilinganishwa na haiku uliotangulia.

Kwa siku ya pili mtawalio, makundi makubwa ya waandamanaji yalikabiliana na majesty ya ulinzi nje ya Ikulu ya Marekani mini Washington, DC.

Indianapolis ni moja ya miji iliyoshuhudia maandamano ya amani nyakati za mchana lakini yaligeuka kuwa ya vurugu baadae.

Mtu mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi lakini polisi wamesema hakuna afisa yeyote aliyefyatua risasi.

Licha ya amri ya kutotoka nje kutangazwa mjini Philadelphia, polisi 13 walijeruhiwa huku watu watu karibu 35 wakikamatwa huku maduka yakiporwa, magari ya polisi yakichomwa moto na nyumba kacha kuharibiwa.

Amri ya kutotoka nje pia imetangazwa katika miji ya Miami, Portland na Louisville,niongoni mwa miji mingine japo amri hiyo imepuuzwa katika baadhi ya maeneo.

San Francisco nadir mii wa hivi punned kuweka amri ya kutotoka nje, iliyotangazwa na Meya London Jumapili, baada ya mii huo kushuhudia visa vya ghasia na uporaji.

Huwezi kusikiliza tena

Mwendesha mashtaka akizungumzia makosa ya mauaji na kuua bila kukusudia.

George Floyd alikufa vipi?

Ripoti kamili ya madaktari bado haijatolewa lakini malalamishi yanasema kwamba upasuaji uliofanywa kama sehemu ya uchunguzi baada ya kifo cha Bwana Floyd, haukupata ushahidi wowote wa shinikizo la kubanwa kifua au kunyongwa.

Matokeo ya uchunguzi wa daktari yameonesha kwamba Bwana Floyd alikuwa na matatizo ya moyo na mchanganyiko wa yote hayo mawili, pengine vichocheo fulani katika mfumo wake na kukandamizwa na maafisa huenda kulichangia kifo chake.

Ripoti inasema kwamba Bwana Bwana Chauvin aliweka goti lake juu ya shingo ya Bwana Floyd na kumkandamiza kwa dakika 8 na sekunde 46 – karibia dakika tatu ambapo Bwana Bwana Floyd hakuamka tena.

Karibia dakika mbili kabla ya kuondoa goti lake maafisa wengine waliangalia kiganja cha mkono cha Bwana Floyd ikiwa bado mapigo ya moyo yapo lakini hawakuona chochote.

Alipelekwa katika Kituo cha Matibabu kaunti ya Hennepin kwa kutumia ambulansi na kusemekana kwamba amekufa karibia saa moja baadae.

Trump alisema nini?

Akiwa katika Ikulu ya Marekani Ijumaa, Rais Donald Trump alitaja tukio hilo kama baya zaidi kutokea na kusema kwamba amezungumza na familia ya Bwana Floyd, aliyoieleza kama familia ya watu wazuri mno.

Alisema ametoa wito kwa idara ya haki kuharakisha uchunguzi iliyotangaza Ijumaa wa kutathmini ikiwa kuna ukiukaji wowote wa haki uliotekelezwa katika kifo cha Bwana Floyd.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Rais alisema pia wanaopora mali za watu hawastahili kuharibia wengine wengi ambao wanafanya maandamano yao kwa njia ya amani.

Awali alielezea wanaopora mali kama wahuni wanaokosea heshima kumbukumbu ya Bwana Floyd.

Aidha mtandao wa kijamii wa Twitter umemshtumu Bwana Trump kwa kusifia ghasia katika ujumbe wake alioandika: “Uporaji wa mali ukianza, ufyatuaji wa risasi unaanza.”

Watu wamechukulia vipi tukio hili?

Familia ya Bwana Floyd na wakili wake, Benjamin Crump, ilisema kukamatwa kwa Floyd kunaruhusiwa lakini hilo limepitwa na wakati.

Familia hiyo ilisema inataka mshtakiwa ashtakiwe kwa makosa ya mauaji kiwango cha kwanza pamoja na kukamatwa kwa maafisa wengine waliokuwepo.

Taarifa hiyo pia inataka mji huo kubadilisha sera yake, ikisema: “Leo, familia ya George Floyd inalazimika kuelezea kwa watoto wake kwanini baba yao aliuawa na polisi kupitia video iliosambaa mtandaoni.”

Aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama pia nae alitoa maoni yake na kusema: “Hili halistahili kuwa jambo la kawaida kwa Marekani ya 2020.”

Katika taarifa yake aliongeza: “Ikiwa tunataka watoto wetu kukua katika taifa lenye maadili ya juu, tunaweza na nilazime tuwe na maadili mema.”Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *