Korea Kaskazini kutobadili msimamo kufuatia mazungumzo yake na Marekani


Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Korea Kaskazini Ri Yong Ho

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Korea Kaskazini Ri Yong Ho

Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Korea Kaskazini amesema msimamo wa nchi yake hautabadilika hata ikiwa Marekani itataka mazungumzo zaidi.

Ri Yong Hon ameyasema hayo baada ya kumalizika kwa Mkutano kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong- Un, ambayo yalimalizika bila ya makubaliano yoyote.

Rais Trump amesema Marekani imekataa matakwa ya Korea kaskazini ya kutaka kuondolewa kwa vikwazo vyote.

Lakini katika mkutano uliofanywa usiku, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Korea kaskazini Ri Yong Hon amesisistiza kuwa nchi yake ilitaka ilitaka unafuu wa sehemu tu ya vikwazo, na sio kuondolewa vyote.

Amevielezea vikwanzo hivyo ni vile ambavyo vinazuia uchumi na maisha ya watu wao.

Haki miliki ya picha
EPA

Image caption

Waandishi wa Habari walitarajia makubaliano ya viongozi hao

Amesema nchi yake imeweka mapendekezo yenye uhalisia ikiwemo kukiharibu kituo cha utafiti wa nyuklia cha Yongbyon, chini ya uangalizi wa Marekani.

Kwa upande Msemaji wa Ikulu ya Marekani Sara Sanders amesema Rais Donald Trump akiwa njiani kurejea Marekani alizungumza na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe na Rais wa Korea kusini Moon Jae-In.

Aidha Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo amesema anamatumaini kuwa maafisa wa pande zote watayarejesha tena mazungumzo haya, kabla ya kupita muda mrefu.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *