Kwanini hali ya usalama imeendelea kuwa tete nchini DRC?


Rais wa DR Congo Felix Tshisekedi

Mkasa wa hivi karibuni wa kuuawa balozi wa Italia nchini DRC, Luca Attanasio pamoja na walinzi alioandamana nao kutoka mji wa Goma – Kivu ya kaskazini, kumezusha upya mjadala kuhusu usalama au ukosefu wa usalama katika taifa hilo lililoathirika na mizozo ya ndani na vita vya miaka mingi.

Balozi Attanasio alikuwa miongoni mwa watu 7 waliosafiri katika magari mawili ya Umoja wa mataifa WFP kutoka Goma kukagua miradi ya utoaji chakula katika shule kadhaa huko Rutshuru.

Katibu mkuu Antonio Guterres ameshutumu vikali shambulio hilo na kutaka serikali ya Congo ifanye uchunguzi kwa wepesi.

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ilifuatia taarifa hizi kwa kutangaza masharti ya usafiri.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *