Kwanini India inachukulia tendo la ngono kwa ahadi ya kuoa sawa na ubakaji?


Picha inayoonyesha wapenzi wakiwa kwenye ufukwe wa bahari nchini India

Haki miliki ya picha
Getty Images

Ikiwa mwanaume atashindwa kutimiza ahadi ya kumuoa mwanamke , ngono baina ya wapenzi wawili walioelewana inaweza kuchukuliwa kama ubakaji?

Mahakama ya ngazi ya juu zaidi nchini India imetoa jibu la swali hilo na kusema kuwa ni “ndio”.

Katika uamuzi muhimu, mahakama imepitisha uamuzi wa mahakama ya awali na kumtia hatiani daktari kwa kosa la ubakaji katika jimbo la lati la India la Chhattisgarh kwasababu alikuwa na makibaliano ya ya uhusiano wa kingono na mwanamuke baada ya kumuahidi kuwa atamuo, lakini baadaye hakutimiza ahadi hiyo na kumuoa mtu mwingine.

Majaji L Nageswara Rao na MR Shah walisema mwanamke alimruhusu daktari kufanya ngono naye kwasababu aliamini kuwa daktari alikuw ana lengo la kumuoa kwa hiyo haiwezi kuchukuliwa kuwa alimruhusu kufany atendo la ngono kwa hiari.

Bado India ni taifa lenye itikadi za kihafidhina inapokuja katika suala la ngono na mambo yanayohusu jinsia kwa ujumla.

Haki miliki ya picha
BBC/Getty

Mabikra huzawadiwa na mwanamke anayejulikana kuwa aliwahi kufanya tendo la ngono nje ya ndoa huwa inakuwa vigumu kwake kuolewa.

Majaji walisema kuwa mshtakiwa alikuwa na “lengo la wazi ” la kutomuoa , na kuongeza kuwa “tendo la ngono linalofanyika bila dhana halisi haliwezi kuchukuliwa kama hiari “.hata hivyo mahakama ilipunguza kifungo cha miaka 10 alichokuwa amefungwa na mahakama ya mwanzo na kumpa adhabu ya kifungo cha miaka 7 jela , majaji wamesema kuwa ”nilazima akabiliwe na athari za uhalifu alioiutekeleza “.

Hii si kesi ya kwanza – kwa mujibu wa data za serikali za mwaka 2016, polisi walirekodi kesi 10,068 za aina hiyo za ubakaji ”zinazofahamika kama za waathiriwa wa ahadi ya kuolewa”. Mwaka 2015, idaidi ya kesi hizo zilikuwa ni 7,655.

Ubakaji wa mtoto wa miaka 6 ulioitamausha India

Mwathiriwa wa ubakaji wa miaka 13 India aiomba mahakama kutoa mimba

Msichana aliyebakwa aruhusiwa kutoa mimba India

Majaji wa mahakama ya juu zaidi ilishauri mahakama za mwanzo “kuchunguza kwa makini ikiwa kweli mwanamume aliahidi kumuoa muathiriwa au kulikuwa na njama nyingine tangu mwanzo na kwamba alifanya tendo la ngono kwa lengo tu la kuridhisha nafsi yake”.

Hii ina maana kuwa kama mwanaume atathibitisha kuwa kweli alitaka kumuoa mwanamke lakini akabadili nia hiyo baadae , bado haitakuwa ubakaji. Haichukuliwi kama ubakaji ikiwaitabainika kuwa alikuwa na njama mbaya tangu mwanzoni mwa mahusiano yao.

Lakini kama kweli tendo hilo lilifanyika kwa “lengo fulani ” si rahisi kuthibitisha, na uamuzi huachiwa majaji na pia kuna hofu kuwa sheria hiyo inaweza kutumiwa isivyotarajiwa.

Na ukweli ni kwamba ,kutokana na idadi kubwa ya kesi hizo, Jaji Pratibha wa Mahakama ya juu ya Delhi mwaka 2017 alisema kuwa wanawake hutumia sheria za ubakaji wakati wanapokuwa na mahusiano mabaya ya ndoa.

Haki miliki ya picha
Getty Images

“Mahakama hii imeshuhudia mara kadhaa kwamba idai ya ya kesi ambapo watu wote wawili, kwa utashi wao na kupenda kwao, huanza uhusiano wa kimwili, wakati uhusiano unapovunjika kwa sababu fulani mwanamke anatumia sheria kama silaha ya kumuathibu.

” Huwa wanatumia kitendo walichokubaliana kama matukio ya ubakaji labda kutokana na hasira na kuchanganyikiwa, na hivyo kupotosha lengo halisi la sheria zenyewe. hi inahitaji kuwepo na mipaka ya wazi kati ya ubakaji na ngono ya makubaliano, hususan wakati ambapo malalamishi ni kwamba mwanamke alijitolea kufanya ngono kutokana na kwamba aliahidiwa kuwa ataolewa ,”alisema jaji.

Wahindi wengi wanaamini kuwa sheria za ubakaji, hazipaswi kutumika kudhibiti mahusiano ya kujamiiana, hususan ni katika matukio mbapo wanawake Iwana wakala na wanaingia katika mahusiani kwa utashi wao.

Wengi katika mahakama pia wanaonekana kuwa na maoni sawa na haya na kwa kiasi fulani inaelezea ni kwanini idadi ya watu wanaopatikana na hatia kwa kosa hili huwa ndogo na katika kesi nyingi mshtakiwa huondolewa mashtaka.

Haki miliki ya picha
BBC/Getty

Image caption

Mengi kati ya malalamiko ya ubakaji wa kutelekezwa na wapenzi wanaowaahidi kuwaoa hutoka katika familia maskini katika maeneo ya vijijini

Mnamo mwaka 2016, Mahakama kuu ya Bombay ilisema kuwa mwanamke msomi mtu mzima ambaye alikuwa na mahusiano ya ngono ya kukubaliabaadae hawezi kudai amebakwa uhusiano unapokuwa mbaya.

Wakili wa ngazi ya juu na mwanaharakati mwenye makao yake Mumbai- Flavia Agnes, hata hivyo anadai kuwa kile tunachopaswa kukikumbuka ni kwamba mengi kati ya malalamiko haya hutoka katika familia maskini na wanawake kutoka jamii zenye matatizo katika maeneo ya vijijini ambao mara nyingi hulaghaiwa kuingia katika mahusiano ya ngono na wanaume wanaowapa ahadi za uongo za kuolewa na baadae kuwatelekeza mara wapatapo ujauzito.

Aliongeza kuwa chini ya mfumo wa sasa wa sheria, sheria ya ubakajihuenda ndio inayoweza kuwasaidia kudai uharibifu au hata kupewa haki yao

Ndio maana anapendekeza kuwa kipengele cha kutengana chini ya sheria ya ubakaji cha kukabiliana na kesi hizi kitumike badala ya adhabu kali za jela ambapo mwanaume ambaye anapatikana na hatia ya kumlaghai mwanamke anaweza kulipa faini , na kuwajibishw ana malezi ya mtoto atakayezaliwa.



Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *