Maalim Seif apumzishwa hospitalini kutokana na COVID-19Kwa mujibu wa taarifa ya chama cha ACT Wazalendo hali ya Maalim Seif na mkewe zinaendelea vyema kabisa.

Kadhalika ACT Wazalendo imerejea wito wake kwa Watanzania wote kuendelea kuchukua hatua za kujilinda dhidi ya ugonjwa wa COVID-19.

Katika hali ya kuchukua tahadhari zaidi madaktari wamemshauri Maalim Seif kuendelea kuwa chini ya uangalizi maalum katika kipindi chote atakachokuwa anaendelea na matibabu dhidi ya maradhi hayo.

Maalim Seif kuanzia Ijumaa jioni alilazwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja , mjini Unguja, Zanzibar ambako anaendelea kuwa chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari.

Uongozi wa ACT Wazalendo unawataka wanachama wake, Zanzibar na Tanzania bara kumuombea dua Maalim Seif katika kipindi hiki cha kuugua kwake, ili aweze kupona kwa haraka na kurudi kuendelea na majukumu yake.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *