Mabadiliko ya tabia nchi yataleta mzozo wa kimataifa, ripoti ya kiintelijensia ya Marekani inasema


e Chad in 2007

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Chad ni moja ya nchi kadhaa zilizotajwa katika tathmini hiyo kuwa katika hatari ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Mabadiliko ya tabia nchi yatasababisha mzozo wa kimataifa unaondelea, kwa mujibu wa taarifa za kijasusi katika tathimini inayoelezwa kuwa mbaya inayohusu hali ya hewa. Taarifa hiyo ya kwanza ya kiintelijensia kuhusu mabadiliko ya tabia nchi inaangalia athari za mabadiliko ya tabia nchi kwenye usalama kuelekea mwaka 2040.

Mataifa yatazozana kuhusu namna gani ya kushughulikia athari ambazo zitazigusa zaidi nchi masikini, nchi ambazo zina uwezo mdogo wa kukabiliana nazo. Ripoti hiyo pia inaonya juu ya hatari ikiwa teknolojia za uhandisi za jiografia za baadaye zitatumiwa na nchi zingine zikiendelea kusimama peke yake.

Tathimini hiyo ya kurasa 27 zinajumuisha maoni ya taasisi zote 18 za kijasusi Marekani. Ikiwa ni ya kwanza ikiangalia mabadiiko ya tabia nchi na usalama wa taifa hilo. Ripoti hiii inatoa picha kwamba kushindwa kwa dunia kushirikiana, kutapelekea kuwa na ushindani wa hatari na kuyumba. Ripoti hiyo imetolewa muda mfupi kabla mwezi ujao Rais nchi hiyo, Joe Biden kuhudhuria mkutano mkubwa wa mabadiliko ya tabia nchi wa COP26 utakaofanyika huko Glasgow, Scotland kutafuta muafaka wa kimataifa.

Ripoti inaionya kwamba nchi zitajaribu kulinda chumi zao na kufaidika kupitia teknolojia mpya. Baadhi ya nchi zitagomea kuchukua hatua, huku zaidi ya nchi 20 zinategemea nishati ya mafuta kwa zaidi ya asilimia 50% ya mauzo yake ya nje.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *