Majivu yaliyoibiwa yarejeshwa kwa simu ya kilio


Dennis Bebnarz, who died aged 19

Haki miliki ya picha
Kinga Bebnarz

Image caption

Dennis alifariki akiwa na miaka 19; upande wa kulia ni sanduku lililokuwa na majivu yake

Majivu ya kijana mmoja yaliyoibiwa ndani ya gari la familia yake, yarudishwa, baada ya mwizi kuwapigia simu huku akilia.

Familia ya Dennis Bebnarz imesema walipanga kumwaga mabaki ya Dennis katika sehemu yenye utulivu na nzuri baada ya kifo chake.

Walichagua Cyprus lakini sanduku lenye majivu yake liliibiwa nyuma ya gari lao, wakati wenyewe walipoenda kula chakula katika mgahawa.

Mama yake Dennis, Kinga Bebnarza amesema mwizi huyo alimpigia simu akiwa analia na kuomba msamaha kwa kitendo alichokifanya.

Vilevile alimuelekeza sehemu ambayo polisi waliweza kukuta majivu hayo.

Mwaka mbaya wa maisha yako

Sanduku la mbao lililotumika kuhifadhi majivu hayo lilikuwa ndani ya begi la mgongoni, liliibiwa kutoka kwenye gari la familia ya Bebnarz wakati wakiwa wanakula chakula cha mchana katika mgahawa mmoja.

Bwana na bibi Bebnarz, wanaotoka nchini Poland lakini kwa sasa wanaishi Uswidi (Sweden), walisafiri kuelekea Cyprus kuyamwaga majivu ya Dennis.

Wamesema wameshindwa kusherehekea sikukuu ya Krismasi bila mtoto wao, ambaye alifariki dunia katika ajali ya gari miezi mitano iliyopita.

”Tulitaka kwenda sehemu tulivu kufunga mwaka ambao umekuwa sio mzuri kwetu.” Bi Bebnarz aliiambia BBC.

Siku ya Jumapili wanandoa walisafiri kuelekea nchini Poland baada ya kukosa matumaini ya kuyamwaga majivu ya mtoto wao.

Bi. Bebnarz amesema ameuacha moyo wake nchini Cyprus huku akihofia kuwa majivu ya mwanae yametupwa kwenye shimo la takataka au sehemu mbaya zaidi.

Wazazi hao waliamua kutumia vyombo vya habari kuwaomba wezi au mwizi kurudisha majivu ya mtoto wao.

Lakini jambo ambalo lilimshangaza sana ni pale alipopokea simu ya mtu anaedhaniwa kuwa ni mwizi wa majivu hayo siku ya Jumapili akiwa analia.

Alisikika akiomba msamaha mara kwa mara na kumuambia sehemu wanayoweza kukuta sanduku hilo lenye majivu na kuwaatarifu polisi ambao waliweza kulifuatilia na kulikuta karibu na barabara.

Sanduku hilo lilikuwa limeandikwa jina la Dennis likiwa na mwaka wake wa kuzaliwa na wa kufariki dunia: 2000-2019.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Gari liliibiwa karibu na mgahawa uliokuwa pembezoni mwa bahari katika mji wa Limassol

Polisi wamethibitisha kuwa raia watatu wa Cyprus wamekamatwa juu ya wizi huo.

Wanaume wawili na mwanamke mmoja wanakabiliwa na mashtaka yanyohusu ya kuharibu na kuiba kutoka kwenye gari.

”Kuna mwisho mzuri”

Bi. Bebnarza aliiambia BBC kuwa hana kinyongo na mwizi huyo, lakini anatumaini kuwa ”atabadilisha maisha yake”.

”Ana hisia za mwanadamu na moyo mzuri sana” alielezea.

”Kuna mwisho mzuri” aliyasema hayo licha ya hali mbaya wanayopitia na sasa wazazi hao wamepata haueni. Watasafiri kuelekea Cyprus kesho kuchukua majivu ya Dennis.

Na sasa ikiwa boksi limeonekana wanatumaini kumalizia shughuli ya kumwaga majivu hayo pale watakapofika Cyprus hapo kesho.

”Tunahitaji kutuliza hisia zetu kwanza” amesema bi. Bebnarz. ”Sijalala tangu Ijumaa.”

Lakini amesema sasa wanajisikia wamekamilika baada ya kurudishiwa majivu ya mtoto wao.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *