Marekani yawaonya raia wake kutozuru China kufuatia Corona


Marekani na mataifa mengine ya dunia wamezidisha vizuwizi vya usafiri hii leo kuelekea China huku makampuni yakisema yanakabiliwa na matatizo ya ugavi kutokana na virusi vya corona nchini China. Hali hiyo inatokea siku moja baada ya shirika la afya la kimataifa WHO kutangaza hali jumla ya dharura inayosababishwa na virusi hivyo.

Katika wakati ambapo idadi ya waliofariki dunia kutokana na maradhi hayo ya kuambukiza ikifikia watu 213 nchini China, Marekani imewaonya raia wake wasiitembelee nchi hiyo ya bara la Asia, maradhi hayo yalikoanzia  katika mji wa Wuhan, mji mkuu wa jimbo la Hubei.

Japan imewashauri raia wake wafutilie mbali ziara ambazo si muhimu nchini China, waziri wa afya wa Iran anahimiza marufuku yawekwe kwa wasafiri wote wanaotokea China huku Uingereza ikiripoti  kadhia zake mbili za mwanzo za maradhi hayo.

Serikali ya Italia imeamua kutangaza hali ya hatari na kusitisha safari zote za ndege pamoja na China baada ya kutangaza pia kadhia za mwanzo za virusi vya Corona walivyokuwa navyo watalii wawili kutoka China.

Shirika la WHO limeonya hii leo hatua za kufungwa mipaka pamoja na China zitaleta madhara kwasababau zitawalazimisha watu kufasiri kinyume na asheria na kwa namna hiyo kuzidi kueneza maradhi hao ya kuambukiza.

Ujerumani imetuma ndege kuwahamisha raia wake 100 walioko Wuhan.

Ujerumani imetuma ndege kuwahamisha raia wake 100 walioko Wuhan.

“Imetajwa wazi kabisa kwamba vizuwizi vya safari na biashara havikushauariwa na shirika la WHO” amesema msemaji wa shirika hilo Christian Lindmeier katika mkutano na waandishi habari mjini Geneva hii leo.

Urusi, Singapore na Mongolia wameamua kufunga mipaka yao kwa wasafiri wanaotokea China ili kupunguza hatari ya kuenea maradhi hayo.

Shirika la afya la kimataifa linahisi hakuna haja ya kuzuwia shughuli za usafiri paamoja na China na kwamba njia pekee ya kupunguza kitisho hicho n i kuwaruhusu wasafiri kupita katikia vituo maalum vya ukaguzi.

Masoko ya hisa yalitulia kidogo leo baada ya shirika la afya la kimataifa kusifu juhudi za China za kudhibiti virusi vya Corona baada ya msukosuko wa jana kufuatia idadi ya wahanga kuongezeka mno katika nchi hiyo ya pil muhimu kiuchumi ulimwenguni.

Vyanzo: AFP/ReutersSource link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *