Mark Zuckerberg amezitaka serikali kusaidia kuweka sheria wa udhibiti wa taarifa za intaneti


Mark Zuckerberg

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Mark Zuckerberg anataka sheria za pamoja ziwekwe ambazo zitafuatwa na makampuni yote ya teknolojia

Mark Zuckerberg ameandika barua ya wazi akitoa wito sheria ziwekwe ili kufuatilia taarifa za intaneti.

Kwatika waraka wake wazi uliochapishwa na gazeti la Washinton Post Mkurugenzi mkuu wa Facebook anasema kuwa jukumu la ufuatiliaji wa maudhui hatari ni kubwa sana kwa kampuni ya Facebook pekee.

Ametoa wito sheria mpya ziwekwe katika maeneo manne : “maudhui ya kudhuru, maadili ya uchaguzi , uhamishwaji wa data kwenye intaneti.”

Wito wa Facebook unakuja wiki mbili baada ya mtu mwenye silaha kutumia mtandao huo kusambaza video yake moja kwa moja alipokuwa akiushambulia msikiti katika eneo la Christchurch, New Zealand.

“Watunga sheria mara nyingi huniambia tuna mamlaka makubwa juu ya kauli, na kusema ukweli ninakubaliana,” Bwana Zuckerberg aliandika, na kuongeza kuwa Facebook “inabuni bodi huru ili watu waweze kukata rufaa juu ya maamuzi yetu” juu ya kile kinachotumwa na kile kinachoondolewa kwenye mtandao wetu.

Huwezi kusikiliza tena

Facebook imekuwa ikilaumiwa kutodhibiti mitandao yao, sasa wajipanga kuchukua hatua

Anaelezea mpango mpya wa kuweka sheria kama mfumo ambao angependa kuona unatekelezwa na makampuni mengine pia ya teknolojia companies.

Sheria hizi mpya zinapaswa kuwa sawa katika tovuti zote , alisema , ili iwe rahisi kuzuwia “taarifa za kudhuru” zisisambae haraka kwenye mitandao yote

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Zuckerberg anapendekeza sheria za wazi juu ya nani anawajibika kuzilinda taarifa za watu zinapohamishwa kwenye huduma moja na kutumiwa kwenye huduma nyingine

Nini anachokitaka Mark Zuckerberg?

Kwa kifupi Bwana Zuckerberg anatoa wito wa mambo ya fuatayo:

  • Sheria za pamoja ambazo mitandao yote ya habari ya kijamii inahitaji kufuata, kudhiboiti kutekelezwa na kampuni nyingine , kudhibiti kusambaa kwa taarifa za zinazosababisha mathara.
  • Makampuni yote ya teknolojia kutoa ripoti ya wazi kila baada ya miezi mitatu, sawia na ripoti yao ya fedha.
  • Sheria kali ziwekwe kote duniani za kulinda maadili ya uchaguzi , na kuwepo kwa viwango sawa kwa tovuti zote vya kuwatambua wanasiasa.
  • Ziwepo sheria ambazo haziwahusu wagombea na uchaguzi wote, bali wengine zihusu ”maswala yanayoleta mgawanyo wa kisiasa “, na sheria hizo zitumiwe hata nje ya kipindi rasmi cha kampeni
  • Viwepo viwango vya kudhibiti namna kampeni za kisiasa zinavyotumia data kuwalenga wapiga kura kwenye mtandao
  • Nchi zaidi ziweke sheria juu ya taarifa za kibinafsi kama Mwongozo Muungano wa Ulaya ya ulinzi wa data (GDPR), ambao ulianza kutekelezwa mwaka jana.
  • ”Uwekwe mfumo wa dunia ” hii ikimaanisha kuwa sheri ahizi zitakuwa na viwango sawa duniani, kuliko kuwa tofauti kwa kila nchi.
  • Sheria za wazi juu ya nani anawajibika kuzilinda taarihfa za watu zinapohamishwa kwenye huduma moja na kutumiwa kwenye huduma nyingine

Barua ya wazi, ambayo pia itachapishwa katika baadhi ya magazeti ya Ulaya, inatolewa wakati mtandao huo wa kijamii ukikabiliwa na maswali juu ya nafasi yake katika kufichuliwa kwa data katika sakata la Cambridge Analytica kuhusu matumizi mabaya ya data wakati wa kampeni za uchaguzi.

Ukurasa huo pia umekuwa ukikosolewa kwa kushindwa kuzuwia kusambaa kwa picha za mauaji ya Christchurch , ambapo Waislamu 50 waliuawa walipokuwa wakisali.

Video ya mauaji hayo ilichukuliwa moja kwa moja na mshambuliaji kwenye ukurasa wa Facebook tarehe 15 Machi kabla ya nakili zake kutumwa mara milioni 1.5.

Barua ya Bwana Zuckerberg haikutaja matukio haya.

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Facebook imekuwa ikosolewa kwa kushindwa kuzuwia kusambaa kwa picha za mauaji ya Christchurch

Hata hivyo , awali Facebook ilitangaza kuwa inaangalia uwezekano wa kuanzisha masharti juu ya utumwaji wa video za moja kwa moja baada ya mashambulio ya Christchurch.

Siku ya Ijumaa ilianza kuonyesha utambulisho wa matangazo ya kujinadi ya kisiasa kwenye Facebook katika nchi za Muungano wa Ulaya , ikionyesha ni nani anayejitangaza ni pesa ngapi walizolipia na wanawalenga akina nani.

“Ninaamini Facebook ina wajibu wa kusaidia kutatua matatizo haya, na ninasubiri kwa hamu kuyajadili na watungasheria duniani,” Alisema Bwana Zuckerberg.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *