Mashambulio ya kinyesi na moto yauandama upinzani Burundi


Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Serikali ya rais wa Burundi Pierre Nkurunziza inalaumiwa kwa kuuzima upinzani

Katika kipindi cha miezi miwili iliyopita ,zaidi ya ofisi 10 za chama cha upinzani nchini Burundi – Burundi opposition party National Congress for Freedom (CNL) zimekuwa zikiharibiwa ima kwa kuchomwa mto au kupakwa kinyesi cha binadamu.

Muakilishi wa chama hicho ameiambia BBC kuwa vitendo hivyo ni juhudi za kuzuwia demokrasia na kuutisha upinzani, kabla ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2020.

Waziri wa mambo ya ndani wa Burundi hajathibitisha kuhusu vitendo hivyo

Therence Manirambona, msemaji wa CNL ameieleza BBC namna ofisi zao za Bubanza, Cibitoke, Ngozi, Rumonge na Bujumbura zilivyoporwa, kuteketezwa kwa moto ima kupakwa kinyesi cha binadamu.

Image caption

Ofisi ya CNL Gatete iliyopo wilayani Rumonge, magharibi mwa Burundi, ndio ofisi ya hivi karibuni kushambuliwa, kulingana na muwakilishi wa chama hicho

”Ofisi ya CNL Gatete iliyopo wilayani Rumonge, magharibi mwa Burundi, ndio ofisi ya hivi karibuni kushambuliwa kwa vitendo hivyo ambapo ofisi hiyo ilishambuliwa Jumanne Julai, kwa moto ulioteketeza ofisi”, amesema Therence Manirambona.

Mapema mwezi huu, Wachunguzi wa Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kuihusu Burundi walitoa ripoti juu ya ‘ukiukaji mkubwa ‘ wa haki za kibinadamu nchini Burundi, unaoulenga upinzani.

Muwakilishi wa Burundi katika tume ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva aliitaja ripoti hiyo kama ‘waraka wa uongo’.

Bwana Manirambona amesema kwamba “kuzipaka ofisi zao kwa kinyesi cha binadamu ni kitendo cha chuki isiyo ya kufikirika “.

Image caption

Baadhi wa wanachama wa chama cha CNL wakiwa mbele ya ofisi yao iliyoharibiwa

Bwana Manirambona ameelezea kusikitishwa kwake na kwamba katika nchi yenye taasisi nyingi za usalam na upelelezi , hakuna mtu hata mmoja aliyekamatwa au hata kuhojiwa kuhusiana na vitendo hivyo viovu vinavyoendelea kwenye ofisi zao.

“Kwa hili ,tunadhani kwamba hivi ni vitendo vya uchochezi wa kisiasa dhidi yetu, kwasababu ya katika ngazi za mwanzo baadhi ya watu wanasema kwamba CNL isingepaswa kuwa na ofisi katika maeneo yao ” amesema Manirambona.

Ripoti Shirika la Human Rights Watch iliyotolewa mwezi Juni 2019 Maafisa wa serikali ya Burundi na vijana wa Imbonerakure wanahusika na kupigwa,kukamatwa kiholela, kupotea na kuuwawa wapinzani tangu wa kweli mpaka wanaodhaniwa.

Image caption

Ripoti ya Human Rights watch iliwashutumu vijana wa Imbonerakure na viongozi wa serikali za mikoa kuwaandama wanachama wa (CNL) katika mikoa isiyopungua 18

Ripoti hiyo iliwashutumu vijana wa Imbonerakure na viongozi wa serikali za mikoa kuwaandama wanachama wa chama hicho kipya kipya cha “Baraza la taifa kwa ajili ya Uhuru(CNL) katika mikoa isiyopungua minane kati ya 18 bila ya kuhofia adhabu yoyote.

Kulingana na ripoti hiyo, kampeni ya kuwaandama watu wanaotuhumiwa kukipinga chama tawala imekuwa ikiendelea tangu kura ya maoni ya katiba ilipoitishwa Mei mwaka jana. Hata hivyo kampeni hiyo inaonyesha kuzidi makali tangu chama kipya cha upinzani kiliposajiliwa mwezi wa Februari mwaka huu.

Lewis Mudge, mkurugenzi wa Human Rights Watch kwa eneo la Afrika Kati anasema matumizi ya nguvu yanayozidi kukithiri yamesababishwa na hali ya watu kutojali sheria ikiyoko nchini Burundi. Alivitaja visa vilivyoripotiwa kuwa ni sehemu ndogo tuu ya visa vinavyotokea na ambavyo haviripotiwi kutokana na kutokuwepo vyombo huru vya habari na mashirika ya kijamii.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *