Mashambulizi ya ndege za kivita za Israeli Gaza yaua watu 23


Shambulizi la Jumapili ni baya sana tangu kuzuka kwa mapigano wiki iliyopita kati ya Israeli na Hamas.

Mapema leo, Israel ilipiga bomu nyumba ya Yehya Al Sinwar, kiongozi wa juu wa Hamas huko Gaza, katika siku ya saba mfululizo ya mapigano.

Bado haiku bayana kama Sinwar alikuwa nyumbani. Shirika la habari la Associated Press limeripoti kuwa huenda ‘amejificha sehemu nyingine pamoja na viongozi wa juu wa kundi hilo.’

Mashambulizi ya makombora dhidi ya wanamgambo ya kipalestina yataendelea kadri inavyohitajika, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema jana.

Wafanyakazi wakiondoa kifusi cha jengo lililoshambuliwa na ndege za kijeshi za Israeli Jumamosi lililokuwa na ofisi za shirika la habari la The Associated Press, broadcaster Al-Jazeera na vyombo vya habari vinginevyo, mjini Gaza, Jumapili, Mei 16, 2021. (AP Photo/Adel Hana)

Wafanyakazi wakiondoa kifusi cha jengo lililoshambuliwa na ndege za kijeshi za Israeli Jumamosi lililokuwa na ofisi za shirika la habari la The Associated Press, broadcaster Al-Jazeera na vyombo vya habari vinginevyo, mjini Gaza, Jumapili, Mei 16, 2021. (AP Photo/Adel Hana)Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *