Mbio za Kili zafanyika Tanzania licha ya hofu ya Covid 19


Michuano ya mbio za Kili

Mashindano ya 19 ya mbio ndefu za kimataifa za Kili yamefanyika mkoani Kilimanjaro kaskazini mwa Tanzania na kuwaleta Pamoja washiriki zaidi ya 5000 licha ya uwepo wa hofu ya maambukizi ya virusi vya corona ambavyo bado ni tishio kote duniani.Awali waandaaji wa mbio hizo ambazo huvutia watu zaidi ya watu elfu ishirini na tano walitangaza mambo yangekuwa tofauti kiasi mwaka huu kutokana na tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona ikiwemo washiriki kupewa barakoa na kutakiwa kuzivaa wanapokuwa kwenye mikusanyiko mikubwa lakini pia uwepo wa maeneo ya kunawia mikono yenye vipukusi vya kutosha ili kuhakikisha washiriki wa mbio hizo pendwa Afrika mashariki wanakuwa salama muda wote.

Kwa mujibu wa mmoja wa washiriki, Rehema Salum Kachingwe ambaye amekimbia mbio fupi za kilometa 21 anasema awali kabla mbio washiriki wote walisafishwa mikono kwa vitakasa mikono na kutakiwa kuvaa barakoa “mwanzo tulisafishwa mikono nahata tuliporudi pia na tulitakiwa kuvaa barakoa ila baada ya kuanza walio wengi walizivua na hata baada ya kurejea si wote wamevaa barakoa licha ya kwamba wanazo”Washiriki kutoka Kenya walizuiliwa na serikali yao kushiriki mbio hizo ambazo wamekuwa wakiibuka vinara mara kwa mara.

Kwenye taarifa rasmi iliyotolewa na chama cha riadha cha Kenya ilieleza kutokana na uwepo wa maambukizi vya virusi vya corona kote duniani hawatatoa vibali kwa wanariadha wa nchi hiyo kushiriki mbio za Kili 2021 na waliwataka wote kutosafiri kwenda Tanzania kushiriki tukio hilo.Mkurgenzi wa mbio hizo John Bayo amesema wao kama waandaji wamechukua tahadhari zote wakishirikiana na serikali na wanasikitishwa sana washiriki kutoka Kenya kuzuiliwa kushiriki mbio hizo kwani kumewanyima changamoto wanariadha wa ndani na kupunguza hari ya ushindani kwenye mashindano hayo kwa ujumla.

Mataifa mengine kama Uganda washiriki wake walikuwemo na hata baadhi yao kujinyakulia medali za nafasi za juu ikiwemo ile ya mbio fupi za kilomita 21 ambayo Abel Chebet amejinyakulia ushindi baada ya kutumia muda wa saa moja na dakika tatu na sekunde kumi na saba huku nafasi kwanza ya mbio hizo hizo upande wa wanawake ikienda kwa Mtanzania Failuna Matanga.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *