Mhindu akataa chakula alicholetewa na 'dereva Muislamu '


Mteja alikuwa na tatizo na dini ya dereva aliyemletea chakula

Haki miliki ya picha
NURPHOTO/GETTY

Image caption

Mteja alikuwa na tatizo na dini ya dereva aliyemletea chakula

Kampuni ya huduma za mtandaoni za kutafuta na kuwasilisha chakula nchini India -Zomato imesifiwa kwenye mitandao ya kijamii kwa jibu ililotoa kwa mteja wake wa dini ya Hindu ambae alikataa kupokea chakula alichoagiza kwasababu kililetwa na dereva aliyeonekana kuwa alikuwa ni Muislamu.

Akitumia mtandao wake wa Twitter mwanamme huyo anayejiiya @NaMo_Sarkaar aliwaambia wafuasi wake mtandao ni kuwa : ” Nimefuta huduma ya ya kampuni ya @ZomatoIN kwasababu walimtuma dereva ambaye sio Mhindu aniletee chakula, walisema hawawezi kubadilisha dereva na kwamba hawawezi kunirudishia pesa zangu baada ya kuwaambia sitaki tena chakula. Nikawaambia hauwezi kunilazimisha kuchukua chakula mlichoniletea sikitaki usinirudishie pesa futa oda .”

Alituma ujumbe wa pili kwa njia ya Twitter wa picha ya simu ya mazungumzo yake na huduma ya mteja kwenye app akiwataka wabadilishe dereva na kuelezea : “Tuna shravanna sitaki chakula kutoka kwa Muislamu .”

Shravan ni mwezi mtakatifu wa dini ya Hindu uliotengwa maalumu kwa ajili ya muungu wa duni hiyo anayejulikana kama Lord Shiva.

@NaMo_Sarkaar alielezwa kwenye ujumbe kuwa ingemgarimu rupia 237 sawa na dola $3.44 iwapo angefuta oda ya chakula alichokuwa tayari amekiagiza , na angelipia garama hiyo katika eneo la Jabalpur katikati mwa India, wakati huo.

Kwa hiyo aliamua kuhamishia malalamiko yake kwenye mtandao wa Twitter, lakini mtu anayeendesha huduma hiyo kupitia ujumbe wake wa Twitter kwenye ukurasa wa @ZomatoIn alituma ujumbe uliosema : “Chakula hakina dini . Ni dini “, na ujumbe wake ukapendwa na maelfu ya watu ambao pia waliushirikisha kwa watu wengine.

Haki miliki ya picha
TWITTER

Image caption

Zomato India haikuwa na muda kwa mteja aliyekataa kupokea chakula kutoka kwa dereva wa dini nyingine

Muanzilishi wa kampuni Zomato Deepinder Goyal pia alitumia Twitter kuunga mkono msimamo wa kampuni yake , akisema: “Tunajivunia wazo la India – na wateja wetu watukufu wa tabaka mbali mbali na washirika. Hatuombi msamaha kwa kupoteza biashara yoyote inayokuja kwa njia ya maadili yetu .”

@NaMo_Sarkaar aliwaambia wafuasi wake kuwa : “@ZomatoIN inatulazimisha kuchukua vyakula kutoka kwa watu ambao hatuwataki wala hawarejeshi pesa na hawaonyeshi ushirikiano . Ninaondoa hii programu yao ya mtandao na nitajadili suala hili na mawakili wangu.”

Wakati wengi waliojibu ujumbe wa Twitter wa kampuni ya Zomato walionekana kuafiki namna ilivyomjibu mteja huyo, kwa ujumla amekabiliwa na kiwango kikubwa cha ukosoaji , huku wengine kupitia Twitter wakimshauri kujipikia chakula chake mwenyewe, hususani wakati huu wa mwezi mtakatifu wa Hindu.

Mtumiaji wa Twitter anayetumia @kskiyer alijibu ujumbe wa kwanza wa Twitter , akisema : “Takataka kabisa. Kama unampenda sana Shravan, pika nyumbani kwako, usiagize nje.

Nae @Chandral_ alisema : “Unamaanisha unayoyase au ? Je mpishi angekuwa Muislamu? Kama je yule aliyekuandalia oda yako angekuwa ni wa dini ya Sikh? Je kama wangeleta viungo kutoka kwa Mkristo ? Kutoka shambani hadi nyumbani kwako ,chakula kingekuwa hakijaguswa na mtu yeyote. Haupaswi kuwa unaaagiza chakula mtandaoni kama unahofu nacho.”Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *