Miaka 20 nchini Afghanistan: Je Marekani ilifanikiwa ?


Vita vya miaka 20 Afghanistan vimesababisha machungu ya aina yake kwa Marekani

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Vita vya miaka 20 Afghanistan vimesababisha machungu ya aina yake kwa Marekani

Uamuzi wa Biden wa kuondoa wanajeshi wa Marekani kutoka Afghanistan kufikia Septemba 11, 2021 umechukuliwa na mtazamo tofauti kote duniani.

Kuna wale wanachoshikilia kwamba ndio uamuzi stahiki na kudai imekuwa safari ndefu ambayo haikufanikiwa kufikia malengo yake ingawa pia kuna wakosoaji wake ambao wanachukulia kuwa hakukutolewa muda wa kutosha kwa Afghanistan kujitayarisha ipasavyo katika utekelezaji wa jukumu la kujilinda yenyewe kikamilifu.

Wakati huo Biden akiwa makamu rais, alikuwa anaunga mkono usaidizi wa kijeshi na kibinadamu kujenga tena Afghanistan baada ya Marekani kuondoa utawala wa serikali ya wanamgambo wa Taliban kwasababu ya kumuunga mkono kiongozi wa kundi la al- Qaeda Osama bin Laden, mratibu wa shambulizi la kigaidi lililotokea Septemba 11, 2001 nchini Marekani.

Kipindi hicho, Joe Biden alitembelea Afghanstani katika ziara rasmi kukutana na rais wakati huo Hamid Karzai kujadiliana hali nchini humo, lakini walitofautiana na kulingana na waliokuwa karibu, hafla ya chakula cha jioni ilikasitishwa ghafla bila kutarajiwa.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *