Miaka 28 tangu kuuwawa Rais Melchior Ndadaye


Kwa mara ya kwanza shirika la wajane na mayatima wa mauwaji hayo AVOD limewataka waliohusika kuvunja ukimya kwa kuomba radhi na kwamba bao wako tayari kuwasamehe. soma Burundi: Buyoya apewa kifungo cha maisha kwa mauaji ya Ndadaye

Kwa kipindi cha miaka 28 ilopita tangu kuuwawa rais Melchior Ndadaye wa kwanza kuchaguliwa chini ya misingi ya kidemokrasia, wajane na mayatima wa wahanga wa jaribio la mapinduzi la Oktoba 21 mwaka 1993, wamewataka walopanga  na walotekeleza mauwaji hayo kuvunja ukimya.

Ahishakiye Adele mwenyekiti wa shirika hilo la Avod linalowajumuisha wajane na mayatima wa mauwaji ya Oktoba 21 1993 ambaye pia ni mjane wa alokuwa spika wa bunge kwenye utawala wa hayati Melchior Ndadaye amesema umewadia wakati wa kusameheana na kuishi katika mtangamano. soma Burundi yatoa waranti wa kumkamata Buyoya

Mjane huyo anasema fikra yao hiyo ya kusamehe ni lazima kwanza mtu ajitokeze na akiri makosa yake.

Shirika hilo la wajane na mayatima limekaribisha kuona tayari kuliundwa baraza la Ukweli na maridhiano, na kwenye hatua ya kwanza

mahakama iliwahukumu walotekeleza mauwaji hayo ya rais Melchior Ndadaye na washirika wake. Ahishakiye Adele amesema ni yakini kuwa Makabila yote yaliathiriwa na mauwaji yaloisibu Burundi tangu uhuru wake 1962.

Maridhiano

Muelekeo huo wa watu kusameheana umegubika pia hotuba ya askof Mkuu Anatole aloongoza ibada ya misa kwenye siku hii ya kumbukumbu ya mwaka wa 28 tangu kuuwawa rais Melchior Ndadaye na washirika wake wa karibu.

Tarehe hii ya  Oktoba 21 ilikuwa siku mbaya,  mwenge wa upendo ulizima katika nchi hii. Kila tunachotakiwa kufanya ni kuhakikisha

jinamizi hilo halirudi tena na kutokea katika nchi. Tuachane na chuki zisizo koma,  ulipizaji kisasi, Mwenge wa upendo hugeuka Msamaha na tushuhulishwa na haki ya kila raia na hata wageni. Kesi ya walohusika na mauwaji ya rais Melchior Ndadaye na washirika

wake ilikatiwa rufaa kwa tuhuma kuwa iliwalenga walotekeleza huku vigogo waliopanga mauaji hayo wakisalia huru bila kuandamwa na mkono sheria. Hata hivyo tayari wengi yanao tajwa kuwa katika kesi hiyo ikiwa ni pamoja na rais wa zamani Pierre Buyoya  walikwishatoweka.

 

Amida Issa,DW, BUJUMBURA

 

 Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *