Mji wa Delhi : Wanawake wakiislamu wazungumzia vile walivyochomewa nyumba na kuvuliwa nguo


Women and children inside the shelter

Image caption

Wanawake na watoto waliotorokea makazi ya Indira Vihar

Ghasia mbaya za kidini ambazo zimekumba baadhi ya sehemu katika mji mkuu wa India zinadhihirisha wazi kwamba walio katika hatari ya kuteseka katika mapigano yoyote ni wanawake na watoto, ameandika mwanahabari wa BBC mjini Delhi, Geeta Pandey.

Vita hivyo kaskazini mashariki mwa Delhi vimesbabisha zaidi ya watu 40 kufa na waathirika ni wa Wahindu na waislamu.

Kwasababu ya ghasia hizo maelfu ya wanawake na watoto wa Kiislamu wameachwa bila makazi huku hatma yao ikionekana kukosa matumaini.

Katika ukumbi mkubwa eneo la Indira Vihar, wanawake na watoto wengi waliotoroka makazi yao kwasababu ya ghasia wameketi kwenye mikeka. Wanawake wengi ni vijana na wamebeba watoto wao lakini pia kuna wengine ambao wanacheza kwa makundi.

Ukumbi huo ni wa mfanyabiashara wa Kiislamu lakini kwa sasa umebadilishwa kuwa eneo la kuhifadhi wale waliolazimika kutoroka makazi yao.

Wanawake na watoto hapa walikimbia vita ambapo makundi ya raia wa Kihindi walivamia nyumba zao eneo la Shiv Vihar, moja ya maeneo yalioathirika zaidi.

Eneo hilo ambalo linatenganisha Wahindu na Waislamu kwa barabara tu, jamii hizo mbili zimekuwa zikiishi pamoja kwa amani kwa miongo mingi lakini kwa sasa yote hayo yamebadilika.

Haki miliki ya picha
Bushra Sheikh

Image caption

Nasreen Ansari (kushoto) na mama yake Noor Jehan Ansari wamekuwa wakiishi kwenye makazi haya ya muda kwa wiki kadhaa sasa

Nasreen Ansari, ni miongoni mwa wale waliotoroka makazi yao eneo la Shiv Vihar, anasema kwamba yote yalianza Jumanne mchana wakati ambapo wanawake pekee ndio waliokuwa majumbani. Waume zao walikuwa eneo jingine la Delhi la Ijtema, wakihudhuria mkusanyiko wa kidini.

“Tuliona karibia wanaume 50 hadi 60 hivi. Sikujua wao walikuwa ni kina nani na tulikuwa hatujawahi kuwaona hapo kabla,” anasema Nasreen. Walituambia kwamba wamekuja kutulinda kwahiyo tuingie ndani.”

Huku yeye pamoja na wanawake wengine wakichungulia kupitia madirishani, ghafla wakabaini kwamba wanaume hao hawakuja kuwalinda.

Nasreen ana video aliyoichukua kupitia dirishani. Inaonesha baadhi ya wanaume wote walikuwa wamevalia kofia ngumu za helmeti huku wakiwa wamebeba bakora za mbao.

Nasreen anasema wanaume hao walikuwa wanapaza sauti zao wakizungumza maneno ya dini ya Kihindu kwa nguvu kama vile Jai Shri Ram na kukariri maneno yanayosifu mungu wao wa kima.

Mama yake, Noor Jehan Ansari, anasema majirani wa Kiislamu walimpigia simu na kumwambia kwamba nyumba yake imetiwa moto.

“kutoka dirishani kwetu, tuliona nyumba ya jirani mwengine wa Kiislamu pamoja na duka lake la kuuza dawa zikitiwa moto.”

Washambuliaji, anasema waliharibu transfoma ya umeme na usiku ulipoingia eneo lote lilikuwa giza.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Maelfu ya watu wametoroka eneo la Shiv Vihar

“Muda si muda eneo zima linalotuzingira lilikuwa linawaka moto, walikuwa wanarusha mitungi ya gesi wakilenga maduka na nyumba za Waislamu. Nyumba za watu wa dini ya Kihindu zilikuwa haziguswi,” anasema. ” Hatukuwahi kufikiria kitu kama hiki kinaweza kututokea. Makosa yetu ni kwamba sisi tulizaliwa waislamu.”

Nasreen anasema wanawake walipiga simu nyingi tu katika kituo cha polisi. “Kila wakati walituahidi kwamba wangekuwa hapo ndani ya dakika tano.”

Wakati fulani, Nasreen anasema alipigia simu jamaa zao na kuwaambia kwamba hakuna matumaini ya kunusurika usiku ule.

Hatimaye wakaokolewa saa 12 baada ya kuvamiwa wakati ambapo maafisa wa polisi waliwasili na waume zao.

“Tulikimbilia maisha yetu tukiwa tu na nguo kidogo tulizobeba migongoni. Hata hatukuwa na muda wa kubeba viatu,” anasema.

Wanawake wengine kadhaa katika makazi hayo ya muda pia nao wanazungumzia yale waliopitia usiku ule.

Shira Malik, 19, anasema yeye na familia yake walijificha katika nyumba ya jirani. “Tulinaswa katika vita hivyo na mawe yalikuwa yanarushwa kutokea nje.”

Image caption

Shira Malik (kushoto) anasema yeye na familia yake walijificha kwa nyumba ya jirani

Wanawake wengine walikuwa wananipigia simu na kuniambia vile ambavyo wamenyanyaswa kimapenzi. Washambuliaji walisema, ‘Vueni nguo zao na muzipasue’.

Mama mwenye mtoto wa mwaka mmoja alititirikwa na machozi wakati anaelezea vile nguo zake zilivyopasuliwa na wanaume kadhaa walioingia nyumbani kwake.

Mwanamke mwengine, 30, anasema yeye yuko hai kwasababu ya jirani yake wa dini ya Kihindu aliyesema hapa hakuna Mwislamu.

“Jirani yangu aliambia umati uliovamia nyumba yake, huyu ni mmoja wetu. Hakuna mwanamke wa Kiislamu anayeishi hapa. Wavamizi walipoenda nyuma ya nyumba wakanisaidia kutoroka,” anasema.

Ghasia hizo zilianza baada ya mgogoro kidogo tu kuhusu wale wanaounga mkono na wanaopinga sheria mpya tatanishi ya uraia.

Na ndani ya saa kadhaa, mgogoro huo ulikuwa umeathiri majirani wengine wengi ikiwemo eneo la Shiv Vihar na Bustani ya Chaman.

Image caption

Wanawake wengi wanaelezea vile ambavyo siku hiyo kidogo wanyanyaswe kimapenziSource link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *