Mjue ''Simba Mama'' Mwanamke aliyepambana na wabakaji wa binti yake


Nokubonga Qampi

Nokubonga Qampi amekuwa akifahamika kama “Simba Mama ” nchini Afrika sukini baada ya kumuua mmoja wa wanaume watatu waliombaka binti yake na kuwajeruhi watu wengine. Alishtakiwa kwa mauaji – lakini baada ya malalamiko ya umma mashtaka yalifutwa, na akaweza kuweka juhudi zai katika kuhakikisha mwanae anapona majeraha.

Ilikuwa ni usiku wa manane wakati siku ilipomuamsha Nokubonga kutoka usingizini.

Msichana aliyekuwa aimpigia alikuwa kilomita 500 kutoka nyumbani kwake – na akamwambia binti yake , Siphokazi, alikuwa anabakwa na wanaume watatu ambao wote walikuwa wanawafahamu vizuri

Jibu la kwanza la Nokubonga ilikuwa ni kuwapigia simu polisi, lakini hakuna aliyejibu simu yake. Alifahamu fika kwamba iungechukua muda kufika kijijini kwake, eneo lenye uoto wa kijani kibichi lenye milima ya jimbo la Eastern Cape nchini Afrika Kusini.

Alikuwa ndiye mtu pekee ambaye angeweza kumsaidia binti yake.

“Nilikuwa na uoga, lakini nililazimika kwenda kwasababu alikuwa mwanangu ,”alisema.

“Nilikua nafikiria kwamba nitakapofika pale,huenda atakuwa amekufa… Kwasababu aliwafahamu wabakaji wake, na kwasababu walimfahamu na wakafahamu kuwa anawafahamu, huenda wakafikilia kuwa lazima wamuue ili asiende kuwaripoti.”

Siphokazi alikuwa amewatembelea marafiki zake katika kijiji lakini alikuwa amewaachwa peke yake, amelala wakati walipoondoka nje muda wa saa saba za usiku . baada ya hapo wanaume watatu ambao walikuwa wakinywa pombe katika nyumba moja nzee walimshambulia.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Nokubonga akitembea kijijini

Nyumba ya Nokubonga iliyoezekwa kwa nyasi ina vyumba viwili , ambako amekuwa akilala , na jiko ambako alichukua kisu.

“Nilikibeba nilipokuwa ninatembea kuelekea mahali pa tukio kwasababu sikuwa na imani na usalama wangu ,” alisema . “Ilikuwa gizana ilibidi nitumie tochi ya simu yangu ili niweze kuangalia njia .”

Alisikia sauti ya binti yake akipiga mayowe alipokua akikaribia nyumba alipokuwemo . Alipokuwa kiingia chumbani kwake, mwangaza kutoka kwenye simu yake ulimuwezesha kupata picha mbaya ya mwanae akibakwa.

“Niliogopa … Nikasimama tu mlangoni na nikawauliza wanafanya nini . Walipona ilikuwa ni mimi , wakaja na hasira kunifuata, hapo ndipo nilipofikiria kuwa ninahitaji kujilinda, ilikuwa ni hatua ya moja kwa moja ,” anasema Nokubonga

Nokubonga alikataa kuongelea kwa kina ni nini kilichofuata

Haki miliki ya picha
Getty Images

Jaji katika kesi ya Nokubonga dhidi ya wabakaji alisema inaonyesha kuwa “alikuwa na hisia za hasira sana” alipomuona mmoja wa wanaume akimbaka binti yake a, huku wengine wawili wakiwa wamesimama kando huku suruari zao zikiwa kwenye magoti , wakisubiri muda wao ufike.

Judge Mbulelo Jolwana aliendelea kusema kuwa , “Nilimuelewa kwambahasira zilikuwa zimempanda kupita kiasi .”Lakini anachokumbuka leo kuhusu hadithi yake, anakiri kuwa alikuwa na hofu kwake na kwa mwanae- na sura yake inaonyesha huzuni na machungu .

Ni wazi hata hivyokwamba wanaume hao walipomfuata kwa hasira alijilinda kwa kisu – na kwamba aliwadunga kisu walipokuwa wakijaribu kutoroka ambapo hata mmoja wao aliruka kupitia dirishani. Wawili wakajeruhiwa na mmoja akafa hapo hapo.

Nokubonga hakubaki pale kuangalia ni kiasi gani washambuliaji waliumia . Alimchukua binti yake katika nyiumba ya rafiki yake anayeishi karibu.

Image caption

Siphokazi na Nokubongamwezi Januari miezi ,16 baada ya shambulio la kubakwa

Polisi walipofika , Nokubonga alikamatwa na kupelekwa kwenye kituo cha polisi ambako aliwekwa mahabusu

“Nilikuwa ninamfikiria mwanangu ,” alisema . “Sikuwa na taarifa zozote kumuhusu. Lilikuwa ni tukio la kutisha sana .”

Wakati huo huo Siphokazi alikuwa hoispitalini akihofia hali ya mama yake na kufikiria kuwa yuko mahabusu ni jambo lililomsikitisha sana.

Katika kipindi cha miezi 18 baada ya shambulio hilo la ubakaji wameweza walau kuendelea na maisha yao

Buhle Tonisethe, wakili aliyemuwakilisha Nokubonga mahakamani , anakumbuka kuwa wote walionekana kukata tamaa alipokutana nao kwa mara ya kwanza baada ya shambulio

Ni nadra sana kwa Afrika kusini kwa kesi ya ubakaji kushughulikia isipokuwa kutajwa tu kidogo kwenye vyombo vya habari. Huenda hii ikawa ni sehemu ndogo tu ya matukio mengi ya ubakaji nchini humo ambako inakadiriwa kuwa watu 110 hubakwa kwa siku – hali ambayo rais Cyril Ramaphosa hivi karibuni aliitaja kuwa mzozo wa kitaifa.

Baada ya kesi yake kumalizika, aliamua kufichua siri yake ili kuwapa waathiriwa wengine wa ubakaji ujasili

“Ninaweza kumwambia mtu kuwa hata baada ya shambulio la aina ile kuna maisha, unaweza kwenda tena kjatika jamii . Unaweza bado kuishi maisha yako ,”anasema.

Nokubonga pia haonyeshi hasira kama anavyolinganishwa na vyombo vya habari kuwa anausimba

Anamatumaini kuwa wabakaji wa binti yake wataweza kupata mafanikio mazuri maishani mwao . “Ninatumai kwamba watakapomaliza adhabu yao gerezani watarudi wakiwa watu waliobadilika ,” anasema , “kuhadithia tukio na kuwa mfano hai.”Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *