Mkutano wa Trump, Kim wamalizika bila ya kufikia makubalianoLakini shughuli zote mbili hizo zilifutwa kwa haraka kabla ya kipindi cha mchana kuingia, Alhamisi, na kufanya mkutano huo wa pili wa viongozi hao wa nchi mbili kumalizika kabla ya wakati wake.

“Siku zote lazima uwe tayari kutoka nje ya mkutano,” alisema Trump, akiongeza kuwa “Ningeweze kusaini kitu fulani leo” na kuthibitisha, “tulikuwa na makaratasi yako tayari kwa ajili ya kusaini.”

Rais aliongeza kuwa Kim alitaka vikwazo viondolewe kwa ujumla wake na hatukuweza kufanya hivyo,” Trump alieleza katika mkutano na waandishi wa habari huko Hanoi, baada ya mazungumzo hayo kuvunjika.

“Walikuwa tayari kutokomeza silaha za nyuklia kwa kiwango kikubwa ya maeneo tuliyokuwa tunataka, lakini hatukuweza kuondoa vikwazo vyote kwa hilo.” Amesema walizungumzia kutokomeza kituo cha nyuklia cha Yougbyon, lakini jambo lenye ugumu ni eneo jingine la kuibadilisha uranium kuwa bomu la nyuklia.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *