Mmiliki wa jogoo achomwa kisu usawa wa tumbo na nyonga wakati kuku huyo akijaribu kutoroka


Mmiliki wa jogoo alichomwa kisu usawa wa kati ya tumbo na nyonga

Mtu mmoja ameuawa na Jogoo wake aliyekuwa amefungwa kisu mguuni kwa ajili ya mchezo uliopigwa marufuku wa kupambanisha jogoo Kusini mwa India.

Mmiliki wa jogoo alichomwa kisu usawa wa kati ya tumbo na nyonga wakati kuku huyo akijaribu kutoroka. Mwanaume huyo alipoteza maisha akiwa njiani kuelekea hospitali kwasababu ya kupoteza damu nyingi.

Polisi hivi sasa wanawatafuta watu wengine 15 waliohusika kwenye tukio hilo, ambalo lilifanyika kwenye kijiji cha Lothunur jimbo la Telangana wiki hii.

Kuku huyo alishikiliwa katika kituo cha polisi kabla ya kupelekwa shambani.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *