Msanii maarufu wa mtindo wa Rap Kenya Chris Kantai afariki dunia


Chris Kantadda

Haki miliki ya picha
@ChrisKantadda Facebook

Wakenya wanamuomboleza mojawapo ya wasanii nguli katika mtindo wa kufoka au rap, Chris Kantai.

Vyombo vya habari nchini vinaripoti kwamba Chris aliaga dunia Jumatano katika hspitali moja mjini Nairobi alikokuwa anapokea matibabu baada yakuugua kwa muda mfupi.

Msanii huyo rapa Chris Kantai mwenye umri wa miaka 42 inaarifiwa alilazwa tangu Jumatatu wiki hii.

Gazeti moja limemnukuu mwakilishi wa familia ya msanii huyo Bi Wanjiku Thuku, aliyesema kwamba alifariki kutokana na matatizo ya kupumua.

Baadhi ya vibao alivyosifika navyo Chris ni ‘Happy’ alichomshirikisha na ambacho kinachoonekana kama kibao kilichomkaribisha msanii mwenza STL katika tasnia hiyo.

Kantai, alivuma Kenya katika uwanja huo wa muziki wa kufoka kwa kibao chake ‘Huu Ni Nani’ anasifiwa kwa kuwa mojawap oya wasanii walio na talanta kubwa.

Hatahivyo amekuwa nje ya sekta kwa muda, na alijaribu kurudi mnamo mwaka 2016 kwa kushirkiana na mojawapo ya wasanii maarufu katikamtindo huo wa rap Khaligraph Jones katika kibao ‘Ting Badi Malo’.

Wakenya wamemkumbuka msanii huyo na kutuma risala zao za rambi rambi katika mitandao ya kijamii kwa kutumia #ripkantai huku wengine wakikumbuka baadhi ya vibao vyake na kuvsifia kuvuma hadi hii leo.

Msanii Juliani akieleza namna anavyokumbuka wakati mmoja alivyoshindwa na kantai akatika shindano la muziki huo wa kufoka:



Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *