MTN inashutumiwa kuwafadhili Taliban na Al-Qaeda


Afghanistan

Haki miliki ya picha
AFP Contributor

Image caption

Wapiganaji 2,400 wa Marekani wamekufa tangu kuanza kwa mapigano nchini Afghanistan

Mtandao mkubwa zaidi wa simu barani afrika MTN unasema kuwa unafatilia shutuma dhidi yao, ya kuwafadhili na fedha makundi ya itikadi kali ya Afghanistan.

Shutuma hizo zimetolewa na madai yaliyowasilishwa katika mahakama nchini Marekani siku ya ijumaa.

Madai hayo yanasema kuwa kampuni hiyo ilivunja sheria ya kukabiliana na ugaidi wa Marekani.

Kampuni nyingine tano zimehusishwa katika shutuma hiyo.

MTN inadaiwa kutoa rushwa kwa al-Qaeda na Taliban ili wasiweze kuwekeza pesa nyingi kwa ajili ya kulinda mitambo yao maeneo ya Afghanistan.

Unaweza kusoma zaidi

Fedha hizo walizotoa kwa makundi haya ya kigaidi inasemekana zimetumika kwenye mashumbulio Afghanistan kati ya mwaka 2009 hadi 2017.

Pia inasemekana fedha hizo zimekua zikinunua silaha hivyo kuvunja sheria ya kupambana na ugaidi.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

bango la MTN

MTN ni mtandao mkubwa wa mawasiliano barani Afrika na unashika namba 8 kwa duniani kote, ukiwa na watumiaji zaidi ya milioni 240.

Mwaka 2015 kampuni hiyo ililipishwa fidia ya dola bilioni 5 na serikali ya Nigeria baada ya kushindwa kuthibiti laini za simu ambazo hazikusajiliwa, ambapo fidia hiyo baadae ilipunguzwa hadi kufikia dola bilioni 1.7 baada ya kupambana sana kisheria na baadae kuingiliwa na rais Jacob Zuma aliyekua rais wa Afrika Kusini kipindi hicho.

Mwezi February balozi wa zamani wa Afrika Kusini nchini Iran alikamatwa katika mji mkuu Pretoria, kwa shutuma za kuchukua rushwa kutoka MTN ili kuwafanya MTN kushinda leseni ya kufanya shughuli zake nchini Iran.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *