Mwanamuziki Dudu baya ashikiliwa na Polisi Dar es Salaam


Mwanamuziki wa Tanzania Dudu baya

Haki miliki ya picha
Godfrey Tumaini

Image caption

Mwanamuziki wa Bongo flavour Godfrey Tumaini

Mwanamuziki wa Bongo Fleva Godfrey Tumaini maarufu Dudu baya anashikiliwa na Polisi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano.

Dudu baya alikamatwa siku ya Jumatano akishutumiwa kutoa maneno ya kashfa dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Marehemu Ruge Mutahaba.

Godfrey anashutumiwa kutumia mitandao ya kijamii vibaya.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe alilitaka Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kumchukulia hatua msanii Tumaini Godfrey maarufu ‘Dudu Baya’ ambaye alikuwa akimdhihaki Ruge Mutahaba kabla na baada ya kifo chake.

Katika taarifa ya Wizara hiyo iliyotolewa Februari 26,2019 imesema: ‘Waziri Mwakyembe ameelekeza Basata kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kumchukulia hatua msanii Dudu Baya kwa kumdhihaki marehemu,”.

Mitandao ya kijamii kudhibiti maudhui zaidi

Kodi ya mitandao ya kijamii Uganda kuangaliwa upya

Kwa nyakati tofauti, Dudu Baya kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram alikuwa akimdhihaki Ruge akidai amekuwa akiwadhulumu wasanii na kumuombea afe na hata baada ya kifo chake , lakini pia alikuwa akiwashambulia kwa maneno makali wanamuziki wengine ambao walionyesha kupingana na vitendo vyake.

Kitendo cha mwanamuzjiki huyo kilizua gumzo mitandaoni wengine wakisema anatekeleza uhuru wake wa kutoa maoni yake lakini wengine wakikemea kitendo hicho wakikiita si cha kiungwana wala kistaarabu.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *