Mwandishi habari wa Congo aachiwa huru kwa muda


Mwandishi huyo Sosthene Kambidi, anaeufanyia kazi mtandao wa habari wa Actualite.cf na wakati mwingine mashirika ya habari ya kimataifa, alikamatwa wiki tatu zilizopita na kuambiwa anachunguzwa kwa kula njama ya uhalifu, uasi na ugaidi, lakini waendesha mashtaka hawakutoa ufafanuzi zaidi.

Kambidi alichangia kwenye uchunguzi wa kituo cha Redio France International na shirika la Reuters mwezi Desemba 2017, ambao ulifuchua kwamba maafisa wa idara ya usalama ya serikali, walisaidia kupanga safari ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuchunguza ripoti za ukatili katika mkoa Kasai nchini Congo.

Waendesha mashtaka wameachana na uchunguzi wa kula njama, uasi na ugaidi, lakini wanaendelea kuchunguza namna Kambidi alivyoshindwa kutekeleza jambo linalotakiwa.

Msemaji wa jeshi aligoma kuzungumzia kesi hii na mwwendesha mashtaka mkuu wa jeshi hakupatikana kutoa kauli.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *