Mwigizaji Baldwin amuua mwanamke wakati wa uigizaji


Maafisa wanasema mwongozaji wa filamu Halyna Hutchins amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata na mwenzake Joel Souza amejeruhiwa pia katika tukio hilo.

Kamerafrau Halyna Hutchins getötet

Joel Souza amefikishwa katika kituo cha matibabu cha Santa Fe

Afisi ya polisi ya mji wa Santa Fe inasema tukio hilo limefanyika wakati wa uigizaji wa filamu inayoitwa “Rust.”

Maafisa wanasema Baldwin mwenye umri wa miaka 68 na ambaye ameonekana nje ya makao makuu ya polisi akilia, bado hajafunguliwa mashtaka yoyote.

Uigizaji wa filamu hiyo umesitishwa.

Halyna Hutchins getötet

Halyna Hutchins ameuwawa kwa kupigwa risasi

Hii si mara ya kwanza tukio kama hilo kutokea, kwani Brandon Lee, ambaye ni mwanawe aliyekuwa gwiji wa filamu za Kung Fu Bruce Lee, alifariki dunia baada ya kupigwa risasi wakati wa uigizaji wa filamu ya “The Crow.”

Mwaka 1984, mwigizaji Jon-Erik Hexum alifariki baada ya kujipiga risasi ya kichwa wakati wa uigizaji wa filamu ya “Cover Up.”Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *