Nala: Paka msafiri aliyezuru mataifa mengi zaidi duniani


Nala

Wakati mchezaji wa mchezo wa raga Dean Nicholson alipofungasha virago vyake ili kusafiri duniani , alitumai kwamba safari hiyo itabadilisha maisha yake kabisa.

Lakini kile ambacho mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 hakugundua ni kwamba ni rafiki yake wa miguu minne ambaye angebadilisha maisha yake yote.

Dean , mchomaji vyuma kutoka eneo la Dunbar , alikuwa amechoshwa na kazi yake ya kuanzia saa tatu hadi saa kumi na moja kila siku na akaamua kupanda baiskeli yake kwenda kuona ulimwengu.

Maelezo ya picha,

Dean Nicholson alimpenda paka aliyempatia jina Nala

Aliondoka nchini Uskochi na kusafiri kuelekea Amsterdam . Alipitia Ubelgiji , Ugiriki na Switzerland na Itali kabla ya kupanda feri kuelekea Croatia.

Baadaye alisafiri kuelekea Bosnia ambapo ndipo alipokutana na mnyama ambaye aliandamana naye katika safari yake. Dean aliambia BBC Radio ya Uskochi kwamba : Ilikuwa siku ya kawaida. Nilikuwa nakaribia kuingia Montenegro na nilikuwa naendesha baiskeli nikipanda mlima mrefu. Nilisikia paka akilia nyuma yangu. Alikuwa akinifukuza juu mlimani .Hivyobasi nilisimama na nikaendelea kwenda lakini hakuniwacha. Nilimweka mbele ya baiskeli yangu na kujaribu kumfikisha mji uliokuwa mbele yangu.

”Nilimchunguza kuona iwepo amewekwa pogramu fulani. Laini hakuwa amewekewa chochote na alipanda hadi katiak bega langu na kulala na hapo ndio niligundua kwamba atandamana nami katika safari yangu.

Maelezo ya picha,

Just a cat, a bike and the open road

Maelezo ya picha,

Lifti ya magari yanayotumia kamba angani huko batumi Georgia

Mpago wangu kuelekea Thailand kwa haraka uliharibika na Dean aligundua kwamba paka huyo mdogo ambaye alimpatia jina la Nala, alikuwa amembadilisha.

Akizungumza kutoka Austria, alisema: Amenifunza jinsi ya kutulia na kufurahia maisha.

Kuwa naye katika baiskeli yangu mahitaji yake yanapatiwa kipaumbele , na amepunguza kasi ya ziara yangu kwasababau tunasimama njiani na kucheza pamoja. Kwa kweli anapenda kukimbia katika ufuo bahari.

Maelezo ya picha,

Nala ana pasipoti yake

Wawili hao wamesafiri maili 10,000. Dean alilazimika kutengeneza pasipoti ya kumbeba paka huyo na sasa ulimwengu upo mikononi mwao.

Maelezo ya picha,

Wawili hao wanataka kumaliza ziara yao katika ufukwe wa bahari

Dean alisema: Siwezi kupitia Iran na paka huyu kwasababu hawawezi kumuacha kuishi katika hoteli hivyobasi hilo tutalienzi.

Mpango wetu sasa ni kuendesha baiskeli kupitia Urusi.

Kila eneo wanalokwenda Dean na Nala wanavutia watu wengi. Wakaazi wanampenda abiria huyo ambaye anasafiri ndani ya kikapu mbele ya baiskeli na mara nyengine katika bega la Dean iwapo barabara ni mbaya.

Maelezo ya picha,

Nala akiwa katika hoteli ya Special cave huko Kelebek

Maelezo ya picha,

Hakuna chochote ambacho hawezi kujaribu

Watu wanawasimamisha kumuona paka huyo . Nala amesafiri hadi Albania , Ugiriki na kurudi Dunbar.

Wamekuwa wapenzi wakubwa wa mtandao wa kijamii , wakipata wafuasi 800,000 wa instagram na jumbe 1000 kwa siku.

Wafuasi wao 150,000 katika mtandao wa Youtube wanawapatia fedha za kutosha za matangazo ili kuwafanya kuendelea na safari , kufanyia marekebisho baiskeli yao na kununua chakula cha paka huyo.

Dean amesema kwamba wataend likizo ya majira ya baridi nchini Ugiriki ili kufanya kazi katika hifadhi moja ya wanyama, Baadaye wataelekea Urusi wakati wa majira ya joto na kuelekea Thailand.

Nataka kutumiza ndoto yangu ya kukaa baharini na kunywa madafu.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *