Ni wakati wa waarabu kutawala soka duniani?


d

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mohammed bin Salman, mwenyekiti wa PIF, wamiliki wapya wa Newcastle United

Leo Newcastle United ya England ni moja ya vilabu tajiri kabisa duniani. Imenunuliwa wiki iliyopita na Saudi Arabia kupitia mfuko wake wa “Public Investment Fund (PIF) kwa thamani ya £300m na kuhitimisha miaka 14 ya umiliki wa Mike Ashley.

Ununuzi huo wa waarabu hao wenye utajiri wa zaidi ya £320 billion umezua gumzo na makelele, wengi wakiuona haujakaa sawa, kufuatia rekodi ya masuala ya haki za binadamu huko Saudi Arabia.

Inadaiwa vilabu kadhaa vya ligi kuu England vilijaribu kuzuia ununuzi huo huku Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International likataka kukutana na vilabu vya England kuhusu ununuzi huo. Lakini hilo halizuii kuona dhamira ya waarabu hao kwenye soka. Sasa Newcastle inaungana na vilabu kadhaa duniani vinavyomilikiwa na mabilionea wa kiarabu na kuibua swali kubwa, Je ni wakati wa waarabu kulitawala soka la dunia?

1: Kununua vilabu vikubwa vya soka Ulaya 169025Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *