Precision Air: Kenya kuiruhusu kampuni ya ndege kutoka Tanzania licha ya mgogoro


Kenya imesema ina haki za usafiri ambazo hazitaathirika kufuatia mgogoro na Tanzania

Maelezo ya picha,

Kenya imesema ina haki za usafiri ambazo hazitaathirika kufuatia mgogoro na Tanzania

Kenya haitafuta haki za usafiri za kampuni ya ndege yenye makao yake Tanzania Precision Air ambayo itaanza safari zake kuelekea Jijini Nairobi siku ya Alhamisi licha ya mgogoro uliopo ambao umeilazimu Dar es Salaam kusitisha kampuni tatu za ndege kutoka Kenya kuelekea nchini humo kulingana na gazeti la Business Daily.

”Precision Air ina haki za usafiri ambazo hazitaathirika kufuatia mgogoro na Tanzania ”

Kenya haitafuta haki za usafiri za kampuni ya ndege yenye makao yake Tanzania Precision Air ambayo itaanza safari zake kuelekea Jijini Nairobi siku ya Alhamisi licha ya mgogoro uliopo ambao umeilazimu Dar es Salaam kusitisha kampuni tatu za ndege kutoka Kenya kuelekea nchini humo kulingana na gazeti la Business Daily.

Gazeti hilo limemnukuu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya safari za ndege nchini Kenya KCAA Gilbert Kibe akisema kwamba kampuni ya ndege ya Precision ina haki za usafiri ambazo hazitaathirika kufuatia mgogoro uliopo kati ya Kenya na Tanzania.

Kampuni ya Kenya Airways ambayo ilikuwa na haki zake za usafiri kuelekea Tanzania mwanzo wa mwezi huu wakati kampuni hiyo ya ndege ilipoendelea na safari zake za kimataifa, imezuiwa na mamlaka ya Tanzania kuingia nchini humo kama hatua ya ili kulipa kisasi baada ya Kenya kutoiorodhesha Dar es Salaam katika orodha ya mataifa yalio salama.

”Kampuni ya ndege ya Precision ina haki zilizopo na ninachofahamu ni kwamba haitazuiwa kutua Kenya”, alisema bwana Kibe akizungmza na gazeti la Business Daily.

Bwana Kibe alinukuliwa akisema kwamba anaendelea kufanya majadiliano na wenzake wa Tanzania ili kuondoa masharti yaliowekwa na Tanzania .

Tanzania ilizipiga marufuku kampuni tatu za ndege kutoka Kenya kuingia nchini humo kama hatua ya kulipiza kisasi vita vya kibiashara ambavyo vimekuwepo kati ya mataifa hayo kuhusu usimamizi wa mlipuko wa virusi vya corona.

Maelezo ya sauti,

Kenya Airways yafuta safari za ndege

Hatua hiyo iliochukuliwa na Tanzania inajiri baada ya Nairobi , kwa mara ya pili mfululizo, kuiweka Tanzania miongoni mwa mataifa ambayo sio salama na virusi vya corona.

Hatua hiyo ina maana kwamba wasafiri kutoka Tanzania wataendelea kukabiliwa na masharti ya lazima ya kuwekwa katika karantini kwa wiki mbili wanapowasili Kenya ili kuzuia maambukizi ya maradhi hayo.

Wasafiri kutoka mataifa 130, hatahivyo wako huru kuingia nchini Kenya bila masharti yoyote kufuatia hatua ya pili ambapo serikali iliongeza mataifa mengine 90 katika orodha yake ya mataifa yanayostahili kuingia nchini humo.

Hatua hiyo ilikasirisha mamlaka nchini Tanzania ambayo wiki iliopita ilijibu kwa kuzifungia kampuni tatu za ndege ikiwemo, Airkenya Express, Fly540 na Safarilink Aviation kutosafiri katika maeneo yoyote nchini Tanzania.

“Sababu ya uamuzi wa kufungia kampuni tatu za ndege kutoka Kenya ni mgogoro uliopo kati ya mataifa haya mawili, Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya safari za ndege nchini Tanzania TCAA Hamza Johari alithibitisha katika mahojiano na gazeti la Business Daily mjini Dar es Salaam.

”Baadhi ya mataifa yanaruhusiwa kuingia Kenya bila masharti kama hayo licha ya kwamba yana viwango vya juu vya maambukizi ya Covid-19”, alisema bwana Johari.

Kenya na Tanzania katika kipindi cha miaka minne zimekuwa zikizozana kuhusu visa, kodi na haki ya kuingia katika soka kwa biadha kama vile sukari na maziwa.

Hatua hiyo imeathiri biashara kati ya mataifa hayo mawili, na kusabavisha misururu ya mikutano ikiwemo mkutano wa Arusha kutoka mwezi Novemba 12-16 mwaka uliopita ili kujaribu kuimarisha uhusiano .

Afisa mkuu mtendaji wa shirika la ndege la Kenya Airways Allan Kilavuka alisema kwamba njia ya kuelekea Tanzania inasalia kuwa muhimu kutokana na idadi ya wateja inaowaleta Kenya kwa safari nynegine za kimataifa kwa kutumia ndege za kampuni hiyo.

Tunatumai kwamba tatizo hili litatatuliwa haraka iwezekanavyo , alisema bwana Kilavuka.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *