Sahel: Fahamu kwanini Nigeria,Mali,Burkina faso ,Jamhuri ya kati ,Niger,Chad na Cameroun zinalemewa na makundi yaliyojihami


A regional coalition has recaptured much territory from Boko Haram

Chanzo cha picha, AFP

Mataifa kadhaa ya eneo la Sahel – sehemu ya mataifa kadhaa ya afrika ya kati na magharibi yaliyo jangwani yapo mashakani kwa sababu ya tishio la usalama kutoka kwa makundi mbali mbali yaliyojihami .

Hali hiyo imesababisha maeneo hayo kuwa katika hatari ya kukosa kabisa uthabiti na amani na maelfu ya watu katika nchi kama vile Nigeria , Mali,Chad ,Burkina Faso na Niger wameachwa bila makao .

Ufaransa ambayo imekuwa mstari wa mbele kuzisaidia nchi hizo kukabiliana na makundi mbali mbali ya wapiganaji pia imeonekana kushindwa katika kuleta utulivu katika eneo hilo .

Hali huenda ikawa mbaya zaidi kwa sababu ya kifo cha aliyekuwa rais wa Chad Idriss Deby ambaye alikuwa mojawapo ya viongozi wanaotegemewa kupambana na kundi la Boko Haram ambalo limekuwa likizihangaisha nchi za Nigeria , Chad ,Niger na Burkina faso .Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *