Sandile Shezi: Polisi wamkamata 'milionea mwenye umri mdogo zaidi' Afrika kusini kwa madai ya ulaghai


Mfanyabiashara mwenye umri mdogo zaidi Sindile Shezi

Chanzo cha picha, THULI DLAMINI

Kijana huyu mwenye umri wa miaka 23 Sandile Shezi ambaye anajiita ‘milionea mwenye umri mdogo zaidi’ nchini Afrika Kusini alikamatwa na maafisa wa polisi.

Afisa wa polisi wa eneo la Gauteng nchini Afrika Kusini Mavela Masondo anasema kwamba Shezi alijiwasilisha mwenyewe katika kituo cha polisi akiandamana na wakili wake.

Polisi walimfungulia mashtaka ya ulaghai kijana huyo ambayo alikana.

‘Naweza kuthibitisha kwamba polisi walimkamata kijana huyo. Aliwasilishwa mbele ya hakimu wa eneo la Randburg siku ya Alhamisi ambapo alishtakiwa na mashtaka ya ulaghai’, alisema bwana Masondo.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *