Somalia: Wapiganaji wa Jihadi washambulia ngome ya kijeshi ya Marekani


Baledogle airport in 1992 - payable single online use only

Haki miliki ya picha
Alamy

Image caption

Ngome ya Baledogle, katika picha iliyopigwa mwaka 1992, inatumiwa na vikosi vya Marekani kuwafunza makomando

Wapiganaji wa Jihadiwameshambulia ngome ya kijeshi ambapo askari wa Marekani hutoa mafunzo kwa makomando nchini Somalia , na kusababisha majeruhi, kulingana na taarifa

Wakazi wa eneo hiloo wameripoti kusikia milipuko mizito na milio ya risasi katika uwanja wa ndege wa Baledogle kusini mwa jimbo la Lower Shabelle

Kikundi cha wanamgambo wa al-Shabab kimesema ndicho kilichofanya shambulio hilo , kikitumia mabomu ya kutegwa ndani ya gari kulipua milango kabla ya kuwatuma wapiganaji wake ndani yangome hiyo.

Maafisa w akijeshi wanasema wapiganaji hao wamerudishwa nyuma.

Al-Shabab imesema katika taarifa yake kwamba , ilifanya uvamizi huo na kwamba ulikuwa ukiendelea.

“Baada ya kuvunja uzio wa ngome hiyo yenye ulinzi mkali , mujahideen hao walivamia majengo ya ngome hiyo , na kukabiliana na wanajeshi katika makabiliano makali .”

Ngome hiyo iliyoko umbali wa takriban maili 60 au kilomita 100km (60 miles) west of the magharibi mwa mji mkuu wa Somalia Mogadishu inaaminiwa kuwa makazi ya kikosi maalum cha Marekani, Somalia na walinda amani wa Uganda. Hutumiwa kama kituo cha mashambulizi ya ndege za Marekani zisizo na rubani pamoja na kituo cha mafunzo ya kijeshi yanayotolewa na Marekani nchini Somalia.

Katika tukio jingine, msafara wa jeshi la Italia ulipigwa na mlipuko mjini Mogadishu , imesema Wizara ya ulinzi ya Italia.. Hakuna majeruhi walioripotiwa katika shambulio hilo.

Marekani imeongeza kwa kiasi kikubwa mashambulio yake ya anga dhidi ya Al-shaba, tangu rais Donald Trumpalipochua mamlaka.

Maafisa nchini Somalia wanasema kundi hilo limeongeza mashambulio mjini Mogadishu kama hatua ya kulipiza kisasi dhidi ya mashambulio ya anga ya Marekani.

Mhariri wa BBC Afrika Mary Harper anasema kuwa kutokana na ukweli kwamba al-Shabab waliweza kushambulia maeneo mawili ya kigeni katika siku moja hii inaonyesha kuwa linaratibiwa na ujasusi wa hali ya juu.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani inasema kuwa al-Shabab bado inadhibiti eneo kubwa ya nchi ya Somalia na wanauwezo wa kufanya mashambulio makubwa kwa kutumia mashambulio ya kujitoa muhanga , kwa kutumia vilipuzi na silaha ndogo ndogo.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *