Sweden: Wafahamu viongozi waliodumu madarakani kwa muda mfupi zaidi duniani, wengine mpaka dakika 15


d

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Magdalena Anderson amekuwa waziri mkuu wa aliyeweka historia, ni mwanamke wa kwanza kuwa waziri mkuu na waziri mkuu aliyekaa muda mfupi zaidi.

Magdalena Anderson ameandika historia katika siasa za Sweden na duniani mara mbili kwa siku moja. Kwanza, mapema asubuhi kuelekea mchana, alipata uungwaji mkono mkubwa bungeni kwa kuteuliwa kuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke nchini humo, kabla ya kujiuzulu wadhifa huo mchana na kuweka historia ya kiongozi mkuu aliyekaa madarakani muda mchache zaidi Sweden.

Sweden ndio nchi pekee ya Scandinavia ambayo haijawahi kuongozwa na mwanamke kama kiongozi mkuu wa serikali. Alijiuzulu kwa sababu mshirika wa muungano wa chama chake alijiondoa serikalini na bajeti iliyopendekezwa haikupitishwa. Badala yake, bunge lilipigia kura bajeti iliyopendekezwa na upinzani, ambayo inajumuisha mrengo wa kulia.

“Nilimwambia spika wa bunge kwamba nilitaka kujiuzulu,” Anderson, 54, aliwaambia waandishi wa habari. Aliongeza kuwa ana matumaini ya kujaribu kuwa waziri mkuu tena wakati ujao, lakini tu kwa kuungwa mkono na chama chake.

“Kuna utaratibu wa kikatiba kwamba serikali ya mseto inapaswa kujiuzulu chama kimoja kinapoondoka. “Sitaki kuongoza serikali ambayo uhalali wake utatiliwa shaka,” alisema kiongozi huyo wa chama cha Social Democrats.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *