Tanzania yapigwa marufuku bahati nasibu ya viza Marekani


HABARI ZA HIVI PUNDE

Serikali ya Marekani imepiga marufuku raia wa Tanzania kushiriki katika bahati nasibu wa kupata viza ya kuingia Marekani.

Hatua hiyo inakuja saa chache baada ya serikali ya Trump kumpiga marufuku mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuingia nchini humo.

Bahati nasibu hiyo hutoa viza kwa watu takribani 50,000 kutoka nchi zenye kasi ndogo ya maendeleo kila mwaka kuingia na kufanya kazi Marekani.

Nchi ya Sudani pia raia wake wamepigwa marufuku kuingia katika bahati nasibu hiyo.

Wakati huo huo raia wa nchi nne ikiwemo mbili za Afrika Nigeria na Eritrea wamepigwa marufuku kabisa kuomba viza za kuhamia Marekani.

Marufuku hiyo pia itazihusisha nchi za Myanmar na Kyryzstan.

Hata hivyo raia wa nchi hizo ambao watataka kuingia Marekani kwa kutalii ama biashara wataruhusiwa.

Wiki iliyopita, vyombo vya habari vya Marekani viliripoti juu ya rasimu ya marufuku mpya ya kuingia Marekani kwa mataifa saba.

Ni taifa moja tu la Belarus ambalo lilitajwa katika rasimu ya awali ambalo halijaorodheshwa katika taarifa za leo.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *