Tetesi za soka Jumapili tarehe 31.05.2020: Pogba,Berbatov, Torreira, Sancho,


Manchester imeridhia kumchukua kiungo wa kati Mfaransa Adrien Rabiot, ili Juventus imchukue Paul Pogba

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Manchester imeridhia kumchukua kiungo wa kati Mfaransa Adrien Rabiot, ili Juventus imchukue Paul Pogba

Manchester United wameridhia pendekezo la kiungo wa kati Mfaransa Adrien Rabiot, 25, kujumuishwa katika mpango wa kubadilishana wachezaji, ili Juventus imchukue Paul Pogba, 27. (Calciomercato – via Express)

Manchester United wanaendelea kushauriana na klabu ya China ya Shanghai Shenhua juu ya kurefushwa kwa mkataba wa mkopo wa mshambuliaji wa Nigeria Odion Ighalo,30, hadi Januari 2021. (Goal)

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Dimitar Berbatov ametoa wito kwa klabu hiyo hiyo kutomsajili kiungo wa kati wa Brazili Philippe Coutinho, 27, msimu huu. (Mirror)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Manchester United wanaendelea kushauriana na klabu ya China ya Shanghai Shenhua juu ya kurefushwa kwa mkataba wa Mnigeria Odion Ighalo

Kiungo wa kati wa Arsenal na Uruguay Lucas Torreira, 24, ana ‘ndoto’ ya kujiunga na Boca Juniors licha ya switafahamu kuhusu hatima yake ya baadae. (Fox Sports Argentina, via Evening Standard)

Inter Milan wameweka masharti ‘dhidi ya-Juventus’ katika mkataba wao na Paris St-Germain kumhusu mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi, 27, huku klabu hiyo ya Ufaransa ikipewa masharti ya kulipa £13m ikiamua kumuuza kwa hasimu wao. (Goal)

Manchester United wana imani kuwa watafanikiwa kumsajili mshambuliaji wa England Jadon Sancho, 20, nabla ya msimu ujao, licha ya juhudi za Borussia Dortmund za katakana kumpatia nota huyo mkataba mpya. (90min)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Inter Milan wameweka masharti ‘dhidi ya-Juventus’ katika mkataba wao na Paris St-Germain kumhusu mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi, 27

Stoke City na Preston North End wapo macho baada ya Celtic kukosa kumpatia mkataba mpya winga wa miaka 32- wa Ireland Jonny Hayes. (Mail)

Middlesbrough wake tayari kumuuza beki wao wa miaka, 22- Muingereza Dael Fry, msimu huu lakini klabu hiyo inataka £20m. (90min)

Tetesi bora Jumamosi tarehe 30.05.2020

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Hernandez aliwahi kushinda Kombe la Dunia nchini Urusi

Bayern Munich iko tayari kumtoa mchezaji wake mlinzi Lucas Hernandez, 24, kwa Manchester City wakati inapoendelea na azma yake ya kumwinda winga wa Ujerumani, 24, Leroy Sane. (TZ – via Manchest5r Evening News)

Mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi, 27, anatarajiwa kwamba uhamisho wake hadi Paris St-Germain utakuwa wa kudumu baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya £51.2m na Inter Milan. (Sky Sports)

Aliyekuwa nahodha wa Manchester City Vincent Kompany, 34, amekataa fursa ya kurejea katika klabu hiyo kama msaidizi wa kocha Pep Guardiola muda mfupi baada ya kuondoka ili kutimiza ndoto yake ya kuwa kocha wa Anderlecht. (Sun)

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Kufikia mwisho wa January, Sanchez alikuwa amecheza mara saba katika timu ya Inter Milan msimu huu

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer bado anaweza kuachana na mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez msimu huu huku Inter Milan ikifikiria kuongeza mkataba wake wa makubaliano ya mkopo. (Express)

AC Milan imeonesha nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Burnley na Ireland Jeff Hendrick, 28, katika uhamisho usiokuwa na malipo. (Sky Sports)

Ajenti wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund, 21, Achraf Hakimi, ambaye yuko kwa mkopo kutoka Real Madrid, anasema kipaumbele kwa mchezaji huyo ni kucheza katika klabu ya Uhispania lakini anadai hakuna haraka kwa mchezaji huyo kutoka Morocco kurejea. (Evening Standard)

Haki miliki ya picha
SNS

Image caption

Kristoffer Ajer (kulia)

Leicester City imeimarisha nia yake ya kumsajili mlinzi wa Celtic 22 raia wa Norway Kristoffer Ajer. (Nicolo Schira, via Leicestershire Live)

Kocha wa Birmingham City Pep Clotet anatarajia kwamba angalizo kwa kiungo wa kati kijana Jude Bellingham litaongezeka ikiwa ligi itarejelelewa huku Manchester United na Borussia Dortmund wakihusishwa na mchezaji huyo wa miaka, 16. (Sky Sports)

Arsenal imekamilisha usajili wa winga raia mzaliwa wa Rwanda George Smith, 19, ambaye pia anaruhusiwa kuwakilisha Norway (VG – in Norwegian)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Moussa Dembele ameifungia magoli kumi Lyon msimu huu wa ligi

Aidha, Arsenal imeonesha tena nia kwa mchezaji wa Lyon na mshambuliaji wa Ufaransa Moussa Dembele, 23, na kuchukua hatua ya kuwasiliana na wawakilishi wake. (L’Equipe – in French)

Manchester United itaongeza hamasa zaidi kwa mshambuliaji wa Lyon vilevile ambaye sasa hivi thamani yake inaweza ikapungua. (Star)

Wakati huohuo, Arsenal inatarajiwa kuwafuta kazi watu 10, waliosaidia kutambua mshambuliaji Reiss Nelson, 20, na winga Bukayo Saka, 18, wakati inapoanza kutekeleza hatua za kubana matumizi kutokana na janga la corona. (Mail)Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *