Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 25.11.2021: Mbappe, Bale, Werner, Lacazette, Lingard, Traore, Ziyech


Kylian Mbappe

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kylian Mbappe

Mshambuliaji wa Paris St-Germain na France Kylian Mbappe, 22, anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo wakati kandarasi yake itakapokwisha msimu wa ujao , huku Newcastle united ikiwa miongoni mwa klabu ambayo inawaza kumuwania mchezaji huyo mshindi wa kombe la dunia.(Express)

Winga wa Chelsea na Morocco Hakim Ziyech, 28, na mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner, 25, wanaonekana kama wachezaji mbadala wa winga wa Manchester City na England Raheem Sterling, 26, wanaotarajiwa kujiunga na Barcelona mwezi Januari.(ESPN)

Wito wa Manchester United kutaka kumuajiri mkufunzi wa klabu ya PSG Mauricio Pochettino umekataliwa na klabu hiyo . (Manchester Evening News)

Meneja huyo wa zamani wa klabu ya Tottenham Pochettino , 49 atalazimika kusubiri miezi sita kabla ya kuweza kuwa mkufunzi wa Man United.. (Star)Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *