Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 30.06.2019:Zaha, Pogba, Mbappe, Rabiot, Eriksen, Ndombele, Adams, Morata


Mbappe (kushoto)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Arsenal italazimika kuilipa Crystal Palace pauni milioni 100 kumnasa mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfred Zaha, 26. (Mail on Sunday)

Lakini mwenyekiti wa Eagles, Steve Parish anahofu kuwa kumuuza Zaha kunaweza kuhatarisha mipango yake ya kuwapata wamiliki wapya. (Sun)

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Jacob Bruun Larsen amezivutia timu za Liverpool, Manchester United na Arsenal.(Mail)

Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Daniel Levy amewapigia simu Rea Madrid akitoa ofa ya mchezaji Christian Eriksen, ambaye amekataa kuongeza mkataba wake na Spurs baada ya majira ya joto mwaka 2020. (Marca)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 20, amebakiwa na miaka mitatu katika mkataba wake na Paris St-Germain na hana mpango wa kuongeza mkataba kuendelea kuichezea klabu hiyo. (Marca)

Makamu mwenyekiti wa Manchester United Ed Woodward amewaambia wafanyakazi wake kwa kuwa klabu ina mipango ya kuongeza wachezaji ”vigongo” msimu huu baada ya kumaliza mchakato wa kumnaa Aaron Wan-Bissaka. (Sunday Telegraph)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Paul Pogba atafanya mazungumzo na Kocha Ole Gunnar Solskjae juma lijalo, kuhusu mipango ya kuondoka Old Trafford. (Sun)

Mshambuliaji wa Birmingham City na timu ya taifa ya England Che Adams ameagana na wachezaji wenzake kabla ya kuhamia Southampton. (Mail on Sunday)

Southampton wamekubali kumuuza beki wa kushoto Matt Targett kwa Aston Villa kwa kitita cha pauni milioni 14. (Sunday Telegraph)

Wan-Bissaka ajiunga na Man Utd

Mechi ya mpira iliyosababisha vita

Liverpool na Tottenham wamejiweka mbali na mchakato wa kumchukua Bruno Fernandes, na kumfanya kiungo wa kati wa Sporting Lisbon kujiunga na Manchester Unted. (Sunday Express)

Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino amesema hana kauli ya mwisho kuhusu malengo ya uhamisho.

Spurs wanategemea kumaliza mchakato wa kumnasa kiungo wa kati wa Lyon Tanguy Ndombele, 22 kwa kitita cha pauni milioni 60. (Standard)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Chelsea wameitahadharisha Atletico Madrid kuwa watasitisha mkopo wa mshambuliaji Alvaro Morata, iwapo Atletico Madrid hawatatoa pauni milioni 50 kwa ajili ya uhamisho wa kudumu. (Sunday Telegraph)

Inter Milan inahitaji kukusanya kiasi cha pauni milioni 75 kumnasa mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, kutoka Manchester United, fedha zitakazopatikana baada ya kuumuza kiungo wa kati Joao Mario, 26 na beki wa kushoto Dalbert, 25. (Sun on Sunday)

Mabingwa wa Italia Juventus wameingia makubaliano na Paris St-Germain kumnasa kiungo wa kati Adrien Rabiot. (Sky Italy, Sky Sports)

Mlinda mlango wa Cameroon na Ajax Andre Onana anasema anataka kubaki na timu hiyo ya Uholanzi ingawa Manchester United imekuwa ikionyesha nia kwa mchezaji huyo. (Voetbal International, via Metro)

Watford wamefikia makubaliano kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa timu ya West Brom Craig Dawson kwa kiasi cha pauni milioni 5.5. (Sky Sports)

Millwall na Bristol City watapambana kumnyakua mshambuliaji wa Barnsley Kieffer More.(Mail on Sunday)

Leeds United wanakaribia kumnasa winga wa Wolves, Helder Costa 25.(Birmingham Mail)Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *