Tetesi za soka Ulaya Jumapili 31.01.2021: Ramos, Kounde, Benteke, Dembele, Aurier, Van Aanholt, Tosun


Sergio Ramos yuko tayari kuondoka Real Madrid kuhamia katika timu ya Primia Ligi

Maelezo ya picha,

Sergio Ramos yuko tayari kuondoka Real Madrid kuhamia katika timu ya Primia Ligi

Mlinzi wa Uhispania Sergio Ramos, 34, yuko tayari kuondoka Real Madrid na amesema anataka kuhamia Manchester United. (Mirror)

West Brom wanamtaka mshambuliaji wa Crystal Palace mbelgiji Christian Benkeke, mwenye umri wa miaka 30. (Sun)

Maelezo ya picha,

Kiungo wa kati-nyuma Mfaransa Jules Kounde

Manchester wako makini kusaini mkataba na kiungo wa kati-nyuma Mfaransa Jules Kounde, 22, ambaye alithamanishwa na Sevilla kwa pauni milioni 60 katika uhamisho wa msimu ujao. (Mirror)

Maelezo ya picha,

Serge Aurier alikasirika katika mechi na Liverpool

Kiungo wa kati wa kulia wa Ivory Coast Serge Aurier, 28,anapigania hali yake ya baadaye katika Tottenham baada ya kufoka kwa hasira katika chumba cha kubadilisha mavazi wakati wa mapumziko (half-time) wakati walipofungwa na Liverpool na kuondoka uwanjani baada ya nafasi yake kuchukuliwa na na mchezaji mwingine. (Mail)

Meneja wa La Liga boss Javier Tebas amezishutumu Liverpool na Manchester United kwa kula njama na Fifa na Real Madrid kuhusiana na kombe la Super Ligi la Ulaya. (Sun)

Maelezo ya picha,

Ousmane Dembele akata matumaini ya Manchester United

Winga wa Barcelona mwenye umri wa miaka 23-Mfaransa Ousmane Dembele, ambaye amekuwa akihusishwa na timu ya Manchester United, Chelsea na Juventus, anataka kubaki Nou Camp. (Sport – in Spanish)

Mlinzi wa Newcastle Mmarekani DeAndre Yedlin, 27, yuko tayari kuhamia Galatasaray na atasafiri kuelekea Uturuki kwa ajili ya matibabu baada ya klabu hizo kukubali gharama . (ESPN)

Maelezo ya picha,

Marcos Rojo yuko tayari mkataba wake na Manchester United uvunjwe

Mlinzi wa Argentina Marcos Rojo, 30, yuko tayari mkataba wake na Manchester United uvunjwe ili aweze kujiunga kikosi cha Boca Juniors nchini Argentina kwa mkataba wa bila malipo. (Sky Sports)

Uhamisho wa kiungo wa nyuma-kushoto wa Tottenham na England, Danny Rose kuelekea Trabzonspor unaweza kufeli baada ya upande wa Uturuki kukiri kuwa uhamisho wa kijana huyo mwenye umri wa miaka 30-utakua “mgumu sana ” kutekelezw kwasababu ya masharti ya kudhibiti Covid-19 . (Talksport)

Maelezo ya picha,

Diogo Dalot

AC Milan wanataka kusaini mkataba na kiungo wa kulia-nyuma wa Manchester United Diogo Dalot kwa pauni milioni 15. kijana huyu mwanye umri wa miaka 21 , ambaye ameiwakilisha Ureno katika kikosi cha vinaja walio chini ya umri wa miaka 21, alicheza mchezo mzuri wakati wa mkataba wake wa mkopo . (Sun)

Mshambuliaji wa Everton Mturuki Cenk Tosun, 29 atakuwa Istanbul Jumapili kukamilisha mkataba wake wa mkopo wa kuhamia katika klabu yake ya zamani ya Besiktas. (Sky Sports)

Maelezo ya picha,

Arsenal wanapanga kumhamisha kiungo wa safu ya nyuma Mholanzi Patrick van Aanholt

Arsenal wanapanga kumhamisha kiungo wa safu ya nyuma Mholanzi Patrick van Aanholt mwenye umri wa miaka 30 kutoka Crystal (Mirror)

Liverpool wanamtaka mlinzi wa Arsenal na Germany Shkodran Mustafi, 28, huku wakitaka kusaini mkataba na kiungo wa kati-nyuma kabla ya muda wa mwisho wa uhamisho wa wachezaji kuisha. (Evening Standard)

Maelezo ya picha,

Brandon Williams, 20, hataruhusiwa kuondoka kwa mkopo Manchester United

Kiungo wa nyuma-kushoto wa Manchester United Brandon Williams, 20, hataruhusiwa kuondoka kwa mkopo, anasema meneja Ole Gunnar Solskjaer. Southampton na Newcastle wamekua wakihusishwa na mchezaji huyo wa kimataifa wa England wa kikosi cha vijana walio chini ya umri wa miaka 21 . (Manutd.com)

Newcastle wamewasilisha maombi ya mkopo kwa ajili ya kiungo wa kati wa Celtic Mfaransa Olivier Ntcham mwenye umri wa miaka 24.(Sky Sports)

Maelezo ya picha,

Manchester City hawatasaini mkataba mpya na Edin Dzeko

Manchester City wamekataa fursa ya kusaini upya mkataba na mshambuliaji wa Bosnia-Herzegovina Edin Dzeko, 34, kutoka klabu ya Roma. (Goal)

Preston North End wanataka kusaini mkataba na Mholanzi Sepp van den Berg mwenye umri wa miaka 19 anayecheza safu ya ulinzi ya Liverpool , kwa mkopo . (Football Insider)Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *