Theodore Hall: Jasusi wa Marekani aliyevujisha siri ya nyuklia kwa Sovieti


Picha ya Theodore Hall iliyotumiwa kama utambulisho wake wa kiusalama mjini Los Alamos

Haki miliki ya picha
Los Alamos National Laboratory Handout

Image caption

Theodore Hall alikuwa mwanasayansi mwenye umri mdogo kufanya kazi katika mradi maarufu wa Manhattan ulitengeza bomu la kwanza la atomiki duniani

Agosti 29 mwaka 1949, USSR ilikuwa rasmi “taifa la atomiki” ilipolipua silaha yake ya kwanza ya nyuklia- bomu lililojulikana kama RDS-1.

Serikali za Magharibi ziligutushwa sana suala hilo- kwa mujibu wa rekodi za shirikia la ujasusi la Marekani CIA,, majasusi wa Marekani walifikiria Wasovieti hawangeliweza kutengeneza bomu la nyuklia kabla ya mwaka 1953.

Cha kushangaza ni kwamba ni mwanasayansi wa Marekani, Theodore Hall, aliyeisaidia Moscow kufikia azma yake ya kumiliki silaha za nyuklia kwa kuipatia taarifa Wasovieti

Ni kweli kwamba Theodore Hall hakua raia wa pekee wa Marekani aliyevujisha siri ya uundaji wa bomu la atomiki kwa maadui wa nchi hiyo.

Lakini kilichompatia umaarufu ni jinsi alivyoweza kutekeleza kazi yake kisiri bila kutambuliwa.

Je, mzaliwa huyu wa New-York, aliyesomea sayansi ya nyuklia katika Chuo Kikuu cha Harvard aligeuka vipi kuwa jasusi?

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Wasovieti walilipua bomu lao la katika eneo la Kazakhstan

Haikuwa jambo la kushangaza kuwa bomu la RDS-1 lilifanana sana na bomo la atomiki lililorushwa na Marekani katika mji wa Nagasaki nchini Japan mnamo 9 Agosti 1945

Taarifa za kina kuhusu muundo wa bomu hilo ilifichuliwa kwa Wasovieti kutoka kwa msiri wa ndani wa mradi wa Manhattan, jina fiche lilitotomiwa kuelezea mpango wa uundaji wa silaha za atomiki uiliokuwa unaongozwa na Washington, kwa ushirikiano na Uingereza na Canada.

Siri kubwa

Kuweka siri ilikuwa kigezo kikubwa. kulingana na nukuu ya taarifa ilyochapishwa katika jarida la life magazine mwaka 1945, “Bila shaka ni watu wachache sana kote nchini Marekani waliojua maana halisi ya Mradi wa Manhattan”.

Mmoja wa watu hao alikuwa Theodore Hall.

Alizaliwa Oktoba 20 Mwaka 1925, mamake mzazi alikua mke nyumbani na baba yake alikua mwanabiashara,.

Hall alikuwa nyakati za ngumu sana kimaisha kwa Wamarekani wa kawaidi.

Lakini hali hiyo haikumzuia Hall kufikia malengo yake kimasomo hasa katika somo la hisababi na fizikia.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Moscow iliiba taarifa muhimu kuhusu bomu la atomiki ambalo Marekani ilidondosha jijini Nagasaki mwaka 1945

Akiwa na umri mdogo wa miaka 16,alipata nafasi ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Harvard University, ambako alifuzo mwaka 1944.

Uwezo wake wa kimasomo uligunduliwana maafisa wa Marekani waliokuwa wakitafuta watu watakawaofanyia kazi katika mradi mpya wao nyuklia.

Theodore Hall alihojiwa na kupewa nafasi ya kuhudumu katika maabara ya kisiri ya Los Alamos mwanzoni mwa mwaka 1943.

Lakini kile ambacho maafisa wa Marekani hawakufahamu ni kuwa mwanafizikia hyo mchanga alikuwa amefanyiwa usaili mwingine kama huo.

Hall alikuwa mwanachama wa kundi la wanafunzi wa Harvard wanaoegemea falsafa ya Karl Marx akiwa na mwanafunzi mwenzake aliyefahamika kama Saville Sax.

Sax alikuwa mwana wa kiume wa wahamiaji wa Urusi na alikuwa mfuasi sugu wa Kikomunisti japo alizaliwa na kulelewa mjini New York.

Ukweli ni kuwa Sax ndiye aliyemshawishi Theodore Hall kujiunga na Wasovieti, na kuwa ajenti wa kutoa siri za nyuklia kwa Wasovieti.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Theodore Hall alihofia kile alichotaja kuwa uwezo wa Marekani kuwa wamiliki pekee wa silaha za atomiki

Mwezi Disemba mwaka 1944, mwanasayansi mchanga Hall, kwa ushirikiano na mwanafunzi mwezake wa zamani, walivujisha kwa mara ya kwanza kabisa siri kubwa kutoka Los Alamos – iliyohusisha namna ya kuunda bomu la platoniki.

“Wakati huo mwaka 1944, Nilikuwa na hofu kuhusu hatari ya Marekani kuwa mmiliki pekee wa silaha za atomiki baada ya vita vya dunia,” Theodore Hall alisema katika taarifa iliyoandikwa na kuchapishwa na Gazeti la New York Times mwaka 1997, miaka miwili kabla afariki dunia kutokana na saratani ya figo.

Hall alidai kuwa USSR kumiliki ni njia bora zaidi ya kuidhibiri Marekani

“Muungano wa Sovieti wakati huo haukuwa adui, bali mshirika wa Marekani.” Hall alisema, “Wasovieti walipiganana Wanazi kishujaa, hatua ambayo huenda iliisaidia washirika wake wa Magharibi kutoshindwa.”

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mradi wa Manhattan ulikuwa na uliendeshwa kwa sheria kali na usiri mkubwa

Alijulikana na Wasovieti kama “The Youngster” na aliendelea kuifichulia Moscow siri kuhusu teknolojia ya mawasiliano,hasa jinsi ya kulipua mabomu yalio undwa kwa madini ya plutonium.

Bomu lililodondoshwa na Marekani katika mji wa Nagasaki nchini Japan liliundwa kutokana na madini ya plutonium-tofauti na lile lililolenga Hiroshima,ambalo liliundwa kutokana na madini ya uranium.

Ujumbe wa kisiri

Marekani na USSR huenda walipigana dhidi ya adui mmoja wakati wa vita Vikuu vya Pili vya Dunia, lakini huenda hatua hiyo haikuizuia Moscow na Washington kuchunguzana.

Ukweli wa mambo ni kuwa Marekani katika hatua ya kukabiliana na ujasusi wa Wasovieti ilianzisha mradi uliofahamika kama Venona ambao ulianza kazi mwezi Februari mwaka 1943.

Mwezi Disemba mwaka 1946, majesusi wake walifanikiwa kudukua mawasiliano kutoka NKVD, wizara wa ya mambo ya ndani ya Muungano wa Sovieti.

Mawasiliano ya Wasovieti iliyodukuliwa na Marekani yalibaini kuwa Wasovieti wamekuwa wakichunguza kisiriMradi wa Manhattan.

Haki miliki ya picha
NSA

Image caption

Mamlaka ya Marekani iligundua kuwa Theodore Hall aliwasiliana na Urusi mwaka 1944

Theodore Hall alikuwa akifanyia kazi mradi wake wa PhD katika Chuo Kikuu cha Chicago mwaka 1950, wakati maafisa wa upelelepezi wa Marekani FBI walipombishia mlango.

Alifahamika kama mshirika wa Moscow wa ujumbe wa siri.

Jasusi mwingine wa Los Alamos, alikuwa mwanafizikia wa Ujerumani Klaus Fuchs, ambaye alikamatwa mwaka uliotangulia, baada ya kukiri jukumu lake katika kuwatumia maadui wa siri za nyuklia za Marekani.

Hata hivyo wapelelezi wa FBI hawakupata ushahidi wowote kutoka kwaTheodore Hall, na Saville Sax, ambaye pia alichunguzwa.

Safari ya kwenda Uingereza

Wanasayansi hao hawakupatikana na madai ya kutoa siri kwa Urusi kwasababu uchunguzi haukuonesha ushahidi kwa sababu – Hall hakujihusisha na masuala hayo baada ya mradi wa Manhattan.

Kulikuwa na nyaya za Moscow za mawasiliano ya Moscow ambazo zilitumika kama ushahidi lakini Mamlaka ya Marekani hazikutaka kuzitumia mahakamani, kwasababu hatua hiyo ingelifichua kuwa walidukua mawasiliano ya Wasovieti.

Mwisho wa siku, Hall aliponea mashtaka na wala hakuchukuliwa hatua kama watu wengine waliofungwa jela na na wengine kunyongwa kwa kutoa siri za nchi.

Licha ya hayo Hall na mke wake walihofia usalama wao. Aliachana na wadhifa wake wa kielimu mjini Chicago na kuangazia shughuli za utafiti katika hospitali za New York.

Mwaka 1962, alipata kazi katika Chuo Kikuu cha Cambridge hali iliomfanya kuhamia Uingereza na mke wake.

Image caption

Theodore Hall alifariki kutokana na sratani ya figo mwaka 1999

Theodore Hall alistaafu mwaka 1984 na kuamua kuishi maisha ya kisiri.

Lakini mwaka 1996, mambo aliyofanya zamani yalifichuliwa baada ya mawasiliano kati yake na Urusi kutolewa hadharani.

Wakati huo mashahidi wote waliofahamu mienendo ya Hall walikua wamefariki dunia akiwamo Savile Sax.

”Inadaiwa kuwa niligeuza mkondo wa historia,” Hall aliwaambia waandishi wa New York Times.

“Pengine kama mkondo wa historia haukugeuzwa huenda mngeliongoza vita vya silaha za atomiki kwa miaka 50 – Kwa mfano bomu hilo lingelidondoshwa China mwaka 1949 ama mwanzoni mwa miaka ya 1950.”

“Kwa kweli kama nilifanikiwa kubadili matukio hayo, Nakiri makosa,” alisema.

Hakujawahi kuwa na mashambulio ya nyuklia tangu yalipofanyika mashambulio ya Hiroshima na Nagasaki miaka 74 iliopita na Theodore Hall alifariki akiamini kuwa alichangia kutomika tena kwa silaha hiyo ya maangamizi.



Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *